Katika kuboresha huduma zake kwa wateja, Benki ya
Exim Tanzania leo imezindua huduma mpya zinazolenga kuhamasisha wateja wake na
jamii kwa ujumla kuhusu uwepo wa akaunti zake mpya tatu zinazofahamika kama
Akaunti ya ‘Haba na Haba', Akaunti ya ‘Haba na Haba Plus’ pamoja na Akaunti ya ‘Mzalendo’
zote zikilenga kuwawezesha wateja hao kuhifadhi fedha bila makato ya mwezi kwa
matumizi ya kuweka akiba na kwa shughuli za kila siku.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja jijini Dar es salaam mapema leo,
Mkuu wa Idara ya Amana wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Agnes Kaganda alisema kuwa
huduma hizo zinalenga wateja wote ikiwemo wenye
kipato cha chini, kati na kipato kikubwa.
"Akaunti
hizi za Haba na Haba zinalenga kukidhi mahitaji ya wateja ambao wanahitaji
kuhifadhi fedha zao kwa matumizi ya siku zijazo. Huduma zote zimelenga kutatua
changamoto ya ukosefu wa namna iliyo bora ya kuhifadhi fedha miongoni mwa watanzania
walio wengi bila kuwa na akiba isiyopungua pitia makato ya kila mwezi,’’
alisema.
Aidha, akifafanua
kuhusu akaunti ya Haba na Haba, Bi Agnes Kaganda alisema inawalenga watu wenye nia
ya kuweka akiba kwa ajili ya malengo ya baadae huku akitaja faida zinazombatana
na ufunguaji wa akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kunufaika na kiwango cha juu cha
riba, hakuna makato ya mwezi na huduma ya haraka katika matawi yote ya benki
hiyo,
“Pia inatoa fursa
ya kuweka kiwango chochote cha akiba kwa wateja aidha kila mwezi au kwa muda
wowote ambao wateja wataona ina manufaa kwao katika kutimiza malengo yao, Wateja
wataweza dunduliza akiba zao kupitia simu za mikononi kutoka
Mpesa/Tigopesa/Airtel money/Zantel kwenda kwenye akaunti ya Haba na Haba.’’
alitaja
Ili kufungua akaunti hiyo Bi Agnes
Kaganda alisema mteja anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria
(passport size), nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya
kusafiria, kitambulisho cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi
au kibali cha makazi kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa pamoja
na fedha kiasi cha Tsh 50,000 kama kiasi cha kuanzia.
Akizungumza kuhusiana na akaunti ya
Haba na Haba Plus, Bi Agnes Kaganda alisema inawalenga watu wenye kipato cha
juu ambao pia kupitia akaunti hiyo wataweza kunufaika na viwango vikubwa vya
riba.
“ Akaunti hii pia inalenga kukidhi mahitaji ya wateja ambao wanahitaji kuhifadhi fedha
zao kwa matumizi ya siku zijazo.’’ Alisema huku akitaja faida zitokanazo
na ufunguaji wa akaunti hizo kuwa ni pamoja na kunufaika na kiwango cha juu
cha riba na huduma ya haraka katika matawi yote ya benki hiyo.
“Pia inatoa fursa ya kuweka kiwango chochote
cha akiba kwa wateja aidha kila mwezi au kwa muda wowote ambao wateja wataona
ina manufaa kwao katika kutimiza malengo yao, Kunufaika na riba kubwa jinsi
akiba yako inavoongezeka ikiwa sambamba na huduma zilizoongezwa
thamani kutoka kwa Mameneja wanaohusika na mahusiano ya wateja. Wateja wataweza dunduliza akiba zao kupitia
simu za mikononi kutoka Mpesa/Tigopesa/Airtel money/Zantel kwenda kwenye
akaunti ya Haba na Haba.’’ alitaja
“Pia ili kufungua akaunti hii mteja
anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria (passport size),
nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya kusafiria,
kitambulisho cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi au
kibali cha makazi kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa
pamoja na fedha kiasi cha Tsh 10,000,000 kama kiasi cha kuanzia.,’’ alitaja
Alitaja akaunti ya tatu kuwa ni Mzalendo
akaunti ambayo itawawezesha wateja kupata huduma ya kufanya mihamala ya kila
siku kupitia benki hiyo masaa 24 na siku saba za wiki bila kukatwa malipo ya
kila mwezi na pamoja na kupatiwa ATM kadi
ya malipo bure.
Bi Agnes
Kaganda alizitaja faida za akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kutoa
fursa kwa mmiliki wake kuweza kuindesha bila kuwekewa kiwango cha chini cha
salio, haina ada ya uendeshaji,kupatiwa kadi ya malipo bure pamoja na manunuzi
kwenye maduka yote yenye huduma ya POS (merchant Point of Sale) bila gharama
yoyote.
‘Pia ili kufungua akaunti hii mteja
anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria (passport size),
nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya kusafiria, kitambulisho
cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi au kibali cha makazi
kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa’’ alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...