Charles James, Michuzi TV
HALMASHAURI ya Manispaa ya Wilaya ya Temeke imeweka rekodi kwenye zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura baada ya kuongoza katika kundi maalum lenye idadi ya wapiga kura zaidi ya 90,000.
Uandikishaji wa wapiga kura wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 umevunja rekodi tofauti na miaka iliyopita ambapo wameandikishwa watu milioni 19.6 sawa na asilimia 86
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema hayo leo wakati akitoa tathimini ya zoezi la uandikishaji kwa wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma.
Amesema kwa mujibu wa makadirio ya wapiga kura iliyotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), wananchi wenye sifa ya kupiga kura wanakadiriwa kufikia milioni 26.9 ambapo kati yao wanaume ni milioni 12.8 na wanawake ni milioni 14.1.
Jafo amesema wakati alipotangaza kipyenga cha uchaguzi walikadiria kuandikisha wapiga kura milioni 22 ambao ni sawa na asilimia 85 ya wananchi wenye sifa za kupiga kura ambapo wanaume ni milioni 10.9 na wanawake milioni 11.9.
Amesema kuwa hadi juzi jumla ya wapiga kura milioni 19.6 wamejiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura kwa mwaka 2019 kati yao wanaume milioni 9.5 na wanawake milioni 22.9.
“Idadi hiyo ni sawa na asilimia 86 ya lengo la kuandikisha wapiga kura milioni 22.9.
uandikishaji wa mwaka huu umekuwa wa mafanikio makubwa sana ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2014 ambapo tulikadiria kuandikisha watu milioni 18.7 na waliojitokeza kujiandikisha ni milioni 11.8 sawa na asilimia 63 ya makadirio,”alisema.
Akizungumzia takwimu za uandikishaji wapigakura kimkoa, alisema jumla ya mikoa 26 imeshiriki katika zoezi la uandikishaji ambapo Dar es Salaam ilishika nafasi ya kwanza kuandikisha kwa asilimia 108.
Aidha, mkoa wa Pwani uliandikisha asilimia 96, Mwanza asilimia 95, Tanga asilimia 90, Singida asilimia 90, Morogoro asilimia 89, Mbeya asilimia 83, Ruvuma asilimia 88, Katavi asilimia 88, Mtwara asilimia 86, Dodoma asilimia 85, Rukwa asilimia 85 na Arusha asilimia 85.
Pia, Lindi asilimia 84, Iringa asilimia 84, Mara asilimia 80, Kilimanjaro asilimia 79, Geita asilimia 79, Manyara asilimia 78, Tabora asilimia 78, Songwe asilimia 78, Kagera asilimia 78, Shinyanga asilimia 76, Simiyu asilimia 76, Njombe asilimia 75 na Kigoma asilimia 65.
Ameeleza kuwa ujumla mikoa yote na halmshauri zimefanya vizuri katika uandikishaji wa wapiga kura, kwani hakuna mkoa wala Halmashauri yoyote iliyoandikisha chini ya asilimia 50.
Ametaja mikoa iliyofanya vizuri kuwa ni pamoja na Dar es Salaam asilimia 108, Pwani uliandikisha asilimia 96, Mwanza asilimia 95, Tanga asilimia 90, Singida asilimia 90.
Kwa upande wa halmashauri tano zilizofanya vizuri kuwa ni pamoja na Mlele DC asilimia 152, Ngorongoro DC asilimia 129, Kibiti DC asilimia 126, Temeke asilimia 122 na Monduli asilimia 122.
Jafo amesema halmashauri 5 zilizofanya viziri kuandikisha waandishi wengi zaidi kuwa ni Temeke ambao wameindikisha wapigakura 879,619 (asilimia 122), Ilala iliyoandikisha wapigakura 820,600(asilimia 111) manispaa ya Mwanza iliyoandikisha 224,901(asilimia 105), Ubungo MC imeandikisha 542,728 (asilimia 103) na Kinondoni iliyoandikisha 569872(asilimia 96)
Halmashauri zilizofanya vizuri ni Mlele iliyoanikisha wapigakura 27,196 (asilimia 152), Ngorongoro DC iliyoandikisha 9622 (asilimia 129), Kibiti DC iliyoandikisha 60,539kwaa asiilimia CCmujibu wa idadi ya wapigakura
Akizungumzia changamoto za awali kabla ya kuongeza siku tatu, Jafo alisema baada ya kuanza uandikishaji Oktoba 8 mwaka huu, walibaini changamoto kadhaa.
Ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na hali ya mvua katika baadhi ya maeneo, wananchi kuchanganya na zoezi la uboreshaji wa Dafari la Kudumu la wapiga kura na baadhi ya vituo kuwa mbali na kuwa ngumu kwa wananchi kufikiwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya zoezi la uandikishaji wa wananchi kwenye orodha ya wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba 24 mwaka huu.
Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Rais-Tamisemi wakimsikiliza Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo wakati akitoa taarifa ya zoezi la uandikishaji wananchi kwenye orodha ya mpiga kura leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akimkabidhi Mwandishi wa Michuzi TV, Charles James cheti cha kufanya vizuri kwa Halmashauri ya Monduli. Waziri Jafo aligawa vyeti kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri kwenye zoezi la uandikishaji orodha ya mpiga kura ambapo zawadi hizo zilipokelewa na wandishi wa habari kwa niaba ya Mikoa na Halmashauri hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...