KATIKA kuhakikisha Tanzania inaendesha miradi yake mikubwa inayojengwa sasa na serikali ya awamu ya tano, taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) imepeleka walimu katika miradi hiyo kujifunza kwa vitendo na baadaye wawafundishe wanafunzi uendeshaji na ukarabati.

Baada ya walimu hao kujifunza itasaidia kupata ujuzi na maarifa ya kutosha kurudi kufundisha wanafunzi wa fani mbalimbali chuoni hapo hasa ikizingatiwa chuo hicho kimejikita katika masuala ya sayansi, teknolojia, uhandisi na tafiti.

Aidha, kwa walimu hao kujifunza itasaidia katika kipindi cha uendeshaji miradi kunakua na wataalamu wa kutosha kuendesha na kukarabati bila kutegemea tRNA wataalamu kutoka nje.

Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Mradi Mkubwa waUmeme wa Rufiji (Stiegler’s Gorge) na katika viwanda mbalimbali kupata ujuzi wa kufundishia.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano Viwandani na Mhadhiri  wa Taasisi ya DIT, Dk.John Msumba akizungumza jijini Dar es Salaam amesema mpaka sasa walimu 30 wa fani mbalimbali zinazofundishwa katika taasisi hiyo wamepelekwa katika viwanda na miradi kujifunza kwa vitendo ili kuboresha kile wanachofundisha.

Dk.Msumba amesema kati ya walimu hao 30, sita wapo kwenye mradi huo wa reli ya kisasa
Amesema kutoa wanafunzi mahiri ni muhimu kuwa na wafundishaji mahiri ambapo DIT katika kuboresha elimu wanayoitoa wanaangalia kwa jicho la pekee suala la kuendeleza walimu wake pia.

“Katika kuboresha elimu tunayoitoa tunatazama kwa upande wa wanafunzi pia kwa watumishi wetu ambao ndio wafundishaji, kwa upande wa watumishi tumeanzisha utaratibu wa kuwapeleka katika viwanda na kwenye miradi mikubwa,” amesema Dk.Msumba.

Amefafanua walimu hao  kuna mambo ambayo wanayajua lakini kuna utaalamu mwingine kama vile wa kupasua miamba inahitaji kujifunza kwa ukaribu zaidi  ili itakapohitajika huduma hiyo wakati mwingine hapa nchini tayari tuwe na wajuzi wa kutosha bila kuhitaji kuchukua wataalamu kutoka nje.

“Pia kuna mainjinia ambao wako katika ujenzi wakijifunza kama kupasua miamba, ili tutakapohitaji kujenga miradi ya namna hii tusihitaji tena wageni kutujengea, tukihitaji ukarabati tuwe tunajua nini cha kufanya” ameongeza.

Aidha, amesema baada ya miradi hiyo kukabidhiwa kwa serikali kwaajili ya uendeshaji inabidi kujipanga kuwa na wataalamu katika maeneo mbalimbali ambao watashiriki kuendesha miradi hiyo pamoja na kufanya ukarabati .

“Sisi kama Taasisi tumesema tunataka kushiriki kwa kuandaa wataalamu ili itakapokuja katika uendeshaji wake, utafiti na kutatua matatizo mbalimbali ya kiteknikali tushiriki moja kwa moja," amesema Dk.Msumba.

Malengo ya Taasisi ya DIT ni pamoja na kutoka taaluma bora ya Uhandisi, Utafiti na ushauri wa kitaalamu ndani ya nchi na Afrika Mashariki kiujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...