Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Rajab Abdul 'harmonize'.

MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva Rajab Abdul 'harmonize' amesema ameuza baadhi ya mali zake na kulipa fedha kwa Uongozi wa WBC ili aweze kutumia nyimbo zake kama zamani.

Harmonize ameyasema hayo wakati akihojiwa na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm leo alipokwenda kutambulisha nyimbo yake mpya ya Uno.

Amesema, amefuata sheria ya taratibu za Mkataba, alitakiwa kulipa Milioni 500 na baadhi gharama ambapo hakuwa na fedha ikambidi auze mali zake.

 "Kiukweli kule sijaondoka kwa ubaya, tumefuata sheria na taratibu za mkataba! Nilitakiwa kulipa million 500 na baadhi ya gharama, kiukweli sikuwa na pesa lakini nimeuza baadhi ya mali zangu ili nifanikiwe kulipa hiyo pesa na kwa asilimia kubwa nimelipa bado asilimia chache tu ili niweze kutumia kitu chochote kinachomuhusu Harmonize"

Harmonize amesema kuwa,  mahusiano yake na uongozi wake uliopita hauko sawa, na kuhusu kutokuhudhuria kwa ndoa yake na Mkewe Sarah ni kwa sababu ya nadhiri aliyokuwa ameiweka ya kutaka ndugu zake walioishi vizuri Kijijini kwao ndio wawe wahudhuriaji.

“Sitaki kusema uongo, Mahusiano yangu na uongozi wangu uliopita sio kama zamani, na kuhusu wao kushindwa kuhudhuria ndoa yangu mimi niliweka nadhiri kuwa siku ya ndoa yangu ningependa wahudhuriaji wawe ni ndugu zangu niloishi nao vizuri kijijini”

Akizungumzia msiba wa Ruge, Harmonize amesena nyuma ya Harmonize kuna Rajabu na lazima ahusike kwenye masuala ya kibinadamu   na alikuwa anaumia sana nyimbo zake kutokupigwa kwenye Redio hiyo.

"Mimi ni Harmonize, lakini nyuma yangu kuna Rajabu, Kwenye mambo ya kibinadamu Rajabu lazima ahusike ndio maana nilishiriki kwenye mazishi ya Ruge, Nilichokifanya hakikuniletea matatizo kwenye uongozi wangu uliopita” 

“Amani ndio kitu nilikimiss kipindi ngoma zangu hazipigwi  Clouds, nilikuwa natamani kama hivi nikutane na na nyie tupige story, Naheshimu misingi ya kibiashara lakini sasa tuko good” 

Harmonize ameweka wazi kuwa, "Jembe ni mtu aliyekuwa akinisupport tangu kitambo, Baada ya kuvunja mkataba na lebo yangu ya nyuma! Jembe akaamua kuanza kunisupport japo watu wengi wamekuwa wakimtafsiri vibaya na kuhisi kwamba yeye ndio chanzo cha kunifanya niondoke kule lakini sio kweli”

Harmonize ameanza kufanya ziara ya Vituo vya redio kutambulisha nyimbo yake na kueleza masuala mbalimbali baada ya kuachana na uongozi wake wa zamani WCB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...