Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Mhandisi Isack Kamwelwe (MB) akipata maelezo kwenye banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mda mfupi kabla ya Kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Taifa, Uliohushisha Wadau wa TEHAMA Nchini kutoka Serikalini, Mashirika na Makampuni binafsi Jijini Dar Es Salaam, tarehe 24 Oktoba 2019. Mhe. Kamwelwe alionya watu wenye Uelewa wa TEHAMA kutotumia vibaya ufahamu wao, kwa kuposti taarifa za uzushi na uchochezi zinaweza kuhatarisha Usalama na Amani ya nchi. Alionya, wahusika wote hawatakwepa mkondo wa sheria. (Picha na TCRA).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...