Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kuanza kusikiliza utetezi wa kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wake,  Freeman Mbowe , kwa sababu ya Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya, anaumwa.

Mapema, wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo leo Oktoba 7,2019 imekuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi lakini mshtakiwa Bulaya hayupo.

Mdhamini wa Bulaya, Shukurwa Tungaraza  ambaye alikuwepo mahakamani hapo alidai mshitakiwa Bulaya ni mgonjwa na amelezwa hivyo anahitaji mapumziko kwa siku tatu mfululizo.

Baada ya kueleza hayo, Nchimbi alidai mshitakiwa atakuwa na mapumziko hadi Oktoba 10 na ukizingatia mahakama ilikuwa imepanga kusikiliza kesi hiyo mfululizo kwa wiki hii hivyo, wanaomba isikilizwe Oktoba 11, mwaka huu.

Mapema kabla ya taarufa hiyo ya kuugua Bulaya, wakili wa Utetezi, Profesa Abdallah Safari alidai wanashahidi mmoja ambaye ni Benson Kigaila na kwamba baada ya kujadiliana na upande wa mashitaka wanaomba kesi hiyo ianze kusikilizwa Oktoba 15,17, na 18.

Hakimu Simba alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 15,16 na 18 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Mbunge wa Kawe  Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, katibu mkuu, Vicent Mashinji, mbinhe wa Tarime Mjini Esther Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Wote wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...