Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi umezinduliwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George Simbachawene na kuwaasa wananchi kutunza mazingira, kuacha kukata miti ovyo na kutunza vyanzo vya maji ili nchi isije kuingia kwenye uharibu wa mazingira.
Mkutano huo umeqhudhuriwa na wataalamu mbalimbali wa mazingira na kufanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ukiandaliwa na Chuo Kikuu Dar es Salaam na Kigoda cha Mwalimu Nyerere upande wa Mazingira.
Waziri Simbachawene ameweza kuzindua kitabu kinachojulikana kama Climate Change and Coastal Resources in Tanzania kilichoandikwa kwa ushirikiano na wataalamu kutoka Tanzania, Norway, Marekani na zingine.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Simbachawene amesema mabadiliko ya tabia nchi ni ajenda ya dunia ambapo shughuli za kibinadamu zinasababisha ongezeko la hewa ukaa.
"Hewa ukaa imekuwa inaleta joto na majira yanabadilika na hii inatokana na shughuli za kibinadamu, kiujumla mfumo mzima unabadilika,"
Simbachawene amesema, serikali haina budi kuanza na mfumo mpya wa kutoa elimu ili kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Ameseka, hili ni kongamano la siku mbili litakalotoa mawazo na mtazamo mpya utakaosaidia kupambana na mabadiliko hayo ambapo madhara yatakapozidi kuwa makubwa duniani ongezeko la joto kuongezeka na kufikia 2 bara la Afrika litaingia gharama ya takribani dola Bilioni 530 ili kukabiliana na hali hiyo.
"Wananchi wanatakiwa kutunza mazingira, kuacha kukata miti ovyo, utunzaji wa vyanzo vya maji na hata kutumia nishati mbadala ili mazingira ya kiasili yaendelee kuwapo na kuendelea kufaidika,"
"Utoaji wa elimu ni muhimu kwa wananchi na ukiangalia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 imeweka wazi kila mmoja anahusika kwenye utunzaji wa mazingira na kuyalinda na ili yaweze kuleta tija ya kukuza uchumi kwa kutumia sekta ya viwanda," amesema Simbachawene.
Naye Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mazingira Profesa Pius Yanda amesema kitabu kilichozinduliwa kimeweza kufanyiwa tafiti mbalimbali kwenye ukanda wa bahari na kuandikwa na wataalamu kutoka nchi za Tanzania, Norway na Marekani.
Yanda amesema, kitabu hicho kimeweza kuzungumzia utawala bora utasaidia katika kupunguza athari za tabia nchi na pia kuna makala mbalimbali zilizoandikwa zikizungumzia utafiti wa baharini mabadiliko ya tabia nchi yanavyoweza kuongeza joto na kusababisha upatikanaji mdogo wa samaki.
Kongamano hilo litafanyika kwa muda wa siku mbili na litakuwa na mada mbalimbali zinazozungumzia mabadiliko ya tabia nchi na maelezo yakitolewa na wataalamu wa ndani na nje ya nchi.
Serikali ya Tanzania imeushukuru ubalozi wa Norway kwa kuweza kuwa wadau wakubwa wa mazingira na wamekuwa na mchango mkubwa kwa serikali ya Tanzania kupitia mazingira.

Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George
Simbachawene akizindua kitabu kinachozungumzia mabadiliko ya tabia nchi
kilichoandikwa na wataalamu kutoka Tanzania, Norway na Marekani, mkutano
huo wa kimataifa umeandaliwa na Chuo kikuu Dar es Salaam na Kigoda cha
Mwalimu Nyerere Mazingira. Akiwa sambamba na Naibu Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia Ole Nasha, Makamu Mkuu wa Chuo Prof William
Anangisye na Balozi wa Norway Nchini Tanzania.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George
Simbachawene( kushoto) akipeana mkono na Mwenyekiti wa Kigoda cha
Mwalimu Nyerere Mazingira Prof Pius Yanda baada ya kuzindua kitabu
kinachozungumzia mabadiliko ya tabia nchi kilichoandikwa na wataalamu
kutoka Tanzania, Norway na Marekani, mkutano huo wa kimataifa
umeandaliwa na Chuo kikuu Dar es Salaam na Kigoda cha Mwalimu Nyerere
Mazingira.
Mwenyekiti
wa Kigoda ch Mwalimu Nyerere Mazingira Prof Pius Yanda akizungumzia
kitabu kilichozinduliwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) George Simbachawene kinachoelezea mabadiliko ya
tabia nchini. Mkutano huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...