Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Karibu Tanzania Organization (K.T.O) limetoa vitabu na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 165 kwa ajili ya kufundishia vyuo vya Maendeleo ya wananchi 31 ili kuweza kuongeza utoaji wa elimu katika vyuo hivyo.
Akizungumza katika mafunzo ya wa wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Eusebius Mbonde amesema kuwa vitabu na vifaa ya kufundishia vitumike katika malengo yaliyokusudiwa wanafunzi.
Mbonde amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na shirika la K.T.O kwa muda mrefu ikiwemo katika utoaji wa mafunzo kwa walimu kila baada ya muda kutokana na mahitaji yaliyopo.
Amesema kuwa serikali imekuwa katika uendelezaji wa elimu nchini ikiwemo kwa vyuo vya maendeleo ya wanannchi katika kuhakikisha jamii yote inapata elimu katika mazingira yeyote.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la K.T.O Maggid Mjengwa amesema kuwa vyuo vya maendeleo ya wananchi vilianzishwa mwaka 1975 baada ya Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenda Sweeden ambako alikuta mfumo huo na ndipo aliuleta nchini.
Amesema kuwa shirika limekuwa likifanya kazi na vyuo 31 kati ya vyuo 54 vilivyopo nchini katika program ya elimu haina mwisho kwa utoaji wa mafunzo pamoja na vifaa vya kufundishia.
Mjengwa amesema K.T.O iko mbele katika kupigania elimu nchini kwa vyuo vya maendeleo ya wananchi ili kuhakikisha jamii haichwi nyuma katika kupata elimu hiyo.
Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mtawanya -Mtwara Sophia Mkopi amesema kuwa wanashukuru kwa kupata vitabu pamoja na vifaa mbalimbali ambavyo ni komputa ,Projector .
Amesema kuwa vifaa hivyo watatumia katika vyuo na matokeo yataonekana kwa kwa wananchi kunufaika na elimu na kuweza kusaidia jamii kwa namna moja au nyingine.
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Eusebius Mbonde Akimkabidhi Komputa mpakato
na Projector Mkuu wa Chuo cha Maendeleo
ya Wananchi wa Chuo cha Kasulu FDC Mhandisi Ramadhan Simba ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Eusebius Mbonde akizungumza na waandishi mara baada ya kukabidhi msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali kwa wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi vilivyotolewa na Shirika la Karibu Tanzania Organization (K.T.O) katika mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (K.T.O) Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Shirika hilo katika utoaji wa mafunzo na vifaa mbalimbali kwa wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi katika mafunzo na ukabidhi wa vifaa mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mtawanya mkoani Mtwara Sophia Mkopi akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo yanayotolewa na Shirika la K.T.O pamoja na misaada mbalimbali inayotolewa katika vyuo vya maendeleo ya wanannchi.
Baadhi ya wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi katika mafunzo yanayotolewa na Shirika la K.T.O yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...