Mwamvua Mwinyi, Pwani
KAMPUNI ya uchimbaji wa mawe na kusaga kokoto ya Gulf Aggregates(T), Lugoba imeitaka halmashauri ya Chalinze na serikali kuangalia uwezekano wa kuwashirikisha wawekezaji, kabla ya kufanya mabadiliko ama kuwapandishia ushuru.

Aidha imeiomba halmashauri ya Chalinze, kuboresha miundombinu ya barabara ambayo imekuwa changamoto hususani kipindi cha mvua huku barabara hiyo ikiwa tegemeo la magari ya kokoto zaidi ya 500 yapitayo njia hiyo kila siku.

Akielezea changamoto wanazokabiliana nazo wakati akizungumza na waandishi wa habari ,katika maonyesho ya viwanda yanayoendelea mkoani Pwani, ofisa muajiri wa kampuni hiyo,Agustine Modest alisema,kwasasa halmashauri hiyo imepandisha ushuru kutoka sh.20,000 hadi 60,000 kwa lori kiasi ambacho ni kikubwa kwao .

"Ushuru huu ni mkubwa kwa mwekezaji lakini pia unatuumiza kwani lazima gharama ya kuuza itapanda, tunaomba ushuru upunguzwe hadi sh.30,000 aliomba.

Modest alisema,ushirikishwaji ni muhimu kwakuwa wamekuwa wakipandishiwa ushuru tofauti na faida wanayoipata hivyo kupata hasara.

Nae Ramadhani Siasa ambaye ni meneja masoko wa Lake Gas alieleza, pia wanatarajia kuanza uzalishaji wa mitungi ya gesi ambapo maandalizi yanatarajia kukamilika mwezi desemba mwaka huu.

"Lake gas itakuwa ya kwanza kwa uzalishaji wa mitungi hiyo hapa nchini ambapo awali mitungi yote ilikuwa ikiagizwa kutoka nje ya nchi"alieleza Siasa.

Gulf Aggregates ni kati ya makampuni yanayomilikiwa na Lake Group, makampuni mengine ni Lake gas, Lake Oil, Lake Trans ,Lake petrolium,Lake steel na Lake Cylinders.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...