Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MWITIKIO mdogo kwa wanaochukua na kurudisha fomu za uchaguzi mdogo wa bodi ya ligi Tanzania (TPLB) umepelekea kamati ya uchaguzi ya mpira wa miguu nchini (TFF) kupitia kikao kilichofanyika Oktoba 19,2019 kuongeza siku za kuendeleza zoezi hilo.
kupitia taarifa ilitotolewa na Afisa haari na Mawasiliano wa shirikisho la mpira nchini (TFF) Clifford Mario Ndimbo imeeleza kuwa zoezi hilo la kuchukua na kurejesha fomu litaanza leo Oktoba 21 na kuhitimishwa Oktoba 23, 2019 saa kumi jioni.
Ndimbo ameeleza kuwa maamuzi hayo yamezingatia kanuni 10 (6) ya kanuni za uchaguzi TFF toleo la 2013.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...