Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bara Philip Mangula amezindua kitabu cha The Challenge to China -Tanzania  Relationship to Enhance Cooperation anda Matual Benefits ambacho kimeandikwa na Joseph Kahama ambapo kwa sehemu kubwa kitabu hicho kinazungumzia kwa kina historia ya mwanzo ya urafiki wa hicho.

Wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wamehudhuria tukio la kuzinduliwa kwa kitabu hicho. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam

Akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kitabu hicho Mangula ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, amesema kuwa kwanza anampongeza Kahama kwa uamuzi wa kuandika kitabu hicho na kufafanua kuna Watanzania wengi wanayo mambo mengi lakini hawayaandikii vitabu.

Kuhusu ujumbe uliomo katika kitabu hicho ,Mangula amesema kuwa kinaangalia historia ya mwanzo wa urafiki baina ya nchi ya China na Tanzania ,kikigusia itikadi za kimamba kati ya waanzilishi wa mataifa haya mawili rafiki na kuongeza uhusiano wa nchi hizo pia unatokana  na itikadi za kisiasa za nchi hizi mbili.

"Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, hivyo kuwa karibu na Jamhuri ya Watu wa China chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China .Hivyo uhusiano kati ya Tanzania na vyama hivi viwili si wa chini ya miaka 55.

"Aidha China imetumia miundo ya ufadhili ya 'bila nasharti" au masharti nafuu katika kuufadhili miradi nchini Tanzania,mfano mmoja wapo ni reli ya TAZARA ambayo ni ushirikiano wa Tanzania na Zambia.Shukrani ziwaendee viongozi wetu mzee Kenneth Kaunda na Hayati Mwalimu Nyerere kwa kubaini mradi huu ambao ulikuwa na shabana ya kusaidia nchi ambazo haikuwa na bahari na nchi ambazo zilikuwa zinapigania Uhuru Kusini kwa Afrika,"amesema Mangula.

Ameongeza TAZARA au reli ya Uhuru ni Uwekezaji wa kigeni mkubwa zaidi ambao China imefanya barani Afrika na kwa namna ya pekee nchini Zambia na Tanzania."Ni vema kuwapuuzia wanaodhani mahusiano yetu na China ni kuendeleza ukoloni mambo leo barani Afrika.

"Desemba mwaka 2011 wakati akijibu swali la Mwandishi wa habari kama lililowekwa kama mtego kwa Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete alisema Afrika inahitaji masoko ya bidhaa zake.Afrika inahitaji teknolojia kwa maendeleo yake.China iko tayari kutoa yote haya ,kuna gani kwa hili,"amesema Mangula wakati ananukuu jibu la Rais mstaafu Kikwete ambalo alipoulizwa na Mwandishi wa habari.

Amesema Rais Dk.John Magufuli wa Tanzania pia amedhihirisha msimamo huo Julai mwaka huu wa 2019 wakati wa mkutano huko Kibaha kati ya ujumbe wa Chama cha Kimunisti cha China na vyama vya siasa barani Afrika vipatavyo 40 vyenye itikadi za ujamaa .

Mangula amefafanua kuwa Rais Magufuli alisema " Msingi wa uhusiano wa Tanzania na China na Afrika kwa ujumla ni kuheshimiana kama nchi huru ambazo zinafurahia misaada ya China isiyokuwa na masharti,"

Pia aliongeza kuwa "misaada haitolewi kwa nguvu wala hila ,na hivyo tukiwa na rafiki wa kweli kama China anayeweza kuteleewa ,tunaweza kufikia  mlango yetu,"

Mangula amesema kitabu hicho imetoka wakati nchi yetu inaumiza mahusiano kati ya Taifa letu na nchi nyingine ili kukuza uchumi wetu kulinganna na mpango wa pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano (2016-2021),hivyo basi maudhui ya kitabu hicho hataki nje ya sera ,mwelekeo na juhudi za Serikali yetu ya awamu ya tano ya utawala wetu chini ya Rais Magufuli.

Mangula ameshauri  kuwa Joseph Kahama na Dk.Mduma wameshatoa yaliyopo kwenye kitabu hicho na yeye amejikita  kwenye mapendekezo na hasa kwamba Chama na Serikali waendelee kuweka mazingira bora ya kukuza uhusiano na nchi nyingine.

Kwa upande wake Joseph Kahama ambaye ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kukuza uhusiano wa China na Tanzania ameeleza kwa kina sababu za kuandika kitabu hicho ambacho kitapatikana kwa bei ya Sh.25000 .

Wakati huo huo Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amesema amepata nafasi ya kukisoma kitabu hicho kabla ya kuzinduliwa ambapo amempongeza Mwandishi wa kitabu kwa tafiti ambao ameufanya wakati anaandaa kitabu hicho na yeye alitoa maelezo yake kuboresha kitabu hicho.

Pinda ametumia nafasi hiyo kutoa neno kwa mataifa mkubwa kuwa Tanzania chini ya utawala wa Rais Magufuli umeelekeza nguvu zake katika kujenga uchumi imara ili kufanya nchi yetu kujitegemea badala ya kusubiri misaada.

"Pamoja na urafiki wetu na China na nchi nyingine lakini ukweli lazima tuwe na uwezo wetu wenyewe wa kufanya maendeleo hata hawa wakubwa wenye nguvu tunapokutana kwenye vikao tuwe sawa katika nguvu ya uchumi na bahati nzuri Rais wa China anaamini katika pande zote kuwa sawa,'amesema Pinda.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kitabu hicho,Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke ametumia nafasi hiyo kumpongeza Joseph Kahama na kumuelezea kuwa ni moja ya watu muhimu ambaye amesimama imara kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili na hiyo imefanya awe anakwenda sana China.

Pia amezungumzia uhusiano imara wa China na Tanzania ambao amejikita katika nyanja mbalimbali huku akielezea miradi kadhaa ambayo China imefanya nchini akitolea mfano ujenzi wa reli ya TAZARA, ukumbi wa  mikutano wa Kimataifa  wa Mwalimu Nyerere, Uwanja wa Taifa na miradi mwingine mingi huku akielezea ambavyo raia wa China ambao wameamua kufanya Uwekezaji hapa nchini.
 Mwandishi wa kitabu cha The Challenge to China-Tanzania Relationship to Enhance Cooperation and Mutual Benefits Joaeph Kahama (Kulia) akisaini kitabu kabla ya kumkabidhi Balozi wa China nchini Tanzania(kushoto) .Anayeshuhudia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula akikata utepe katika kitabu hicho ikiwa ni ishara ya kukizindua rasmi.Kushoto ni Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke na kulia ni Mwandishi wa kitabu hicho Joseph Kahama.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula akizungumza wakati akizindua kitabu cha The Challenge to China-Tanzania Relationship to Enhance and Matual Benefits kilichoandikwa na Joseph Kahama ambaye ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kukuza Uhusiano wa China na Tanzania
Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha The Challenge to China-Tanzania Relationship to Enhance Cooperation and Manutal Benefits Philip Mangula(wa nne kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda baada ya kuzinduliwa kwa kitabu hicho.Aliyevaa blauzi nyekundu ni Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...