Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnadani ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnadani wakati alipofika kuzungumza nao ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnadani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma (hayupo pichani) alipofika kuzungumza nao leo


Charles James, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amewaonya wanaume wanaooa watoto wa kike ambao bado ni wanafunzi huku akisema sheria kali itachukuliwa pia kwa wazazi ambao wanalazimisha watoto wao kuolewa.

Akizungumza katika Shule ya Sekondari ya Mnadani wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike, DC Katambi amesema hatokubali kuona binti yeyote anashindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya kuolewa ndani ya Wilaya yake.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imehakikisha inakuza elimu chini kwa kusimamia sera ya elimu bure nchini hivyo wao kama wasaidizi wa Rais Magufuli wana wajibu wa kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bila kujali Jinsia yake.

" Serikali ya Rais Magufuli inapiga vita sana vitendo vya kinyanyasaji vinavyofanywa dhidi ya mtoto wa kike, ni rai yangu kwa jamii zetu kwa ujumla kuilinda haki ya mtoto wa kike isipotee.

Kama Mkuu wetu wa Nchi ametoa nafasi nyingi za kiuongozi kwa wanawake basi ni jukumu letu kuhakikisha watoto wetu wa kike wanapata elimu bora ili kuja kuitumikia Nchi yao katika nafasi mbalimbali, " Amesema DC Katambi.

Amewaonya wazazi wanaoendekeza mila potofu kwa watoto wa kike hasa kwa kukubali kuwaoza wakiwa bado wanafunzi pamoja na kuwafanyia vitendo vingine vya kikatili ikiwemo ukeketaji.

Amesema ili kuwa na Taifa imara lenye uchumi wa kati kupitia viwanda ni lazima pia kukubali kuwanyanyua wanawake na kutupilia mbali mila na tamaduni ambazo hazina tija kwa watoto wa kike.

" Hatuwezi kukubali kuona mabinti zetu wanakosa elimu ambayo Mhe Rais Magufuli ametupatia bure kwa sababu ya tamaa za wanaume ambao wanaoa wanafunzi au kwa mzazi atakayepokea mahari kumuoza binti yake.

Sheria ipo wazi kabisa ole wenu ukutwe na mwanafunzi wa kike, uwe ni Mwalimu, Mfanyabiashara, Mtumishi wa Serikali au Bodaboda tutahakikisha tunakuchukulia. Na yeyote tutakayemkamata atakua mfano kwa wengine, " Amesema DC Katambi.

Amewataka walimu na wanafunzi kushirikiana kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria pale wanapobaini kwamba kuna vitendo vya unyanyasaji na ukandamizaji wanavyofanyiwa watoto wa kike hasa wanafunzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...