Baadhi ya washiriki wa kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu
(hayuko pichani), wakuu wa taasisi, idara na vyombo vya ulinzi
na usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo wakichangia mada
kwenye kikao hicho kilichofanyika Mjini Dodoma jana.

*****************************************

Na Mwandishi Wetu, MOHA

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Jacob Kingu, ametoa wito kwa wakuu wa idara kwenye
taasisi, vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo katika Wizara
hiyo, kutelekeza wajibu walionao ili kuongeza uwajibikaji.

Meja Jenerali Kingu aliyasema hayo Mjini Dodoma jana
alipofanya kikao cha pamoja na wakuu wa idara hizo.

Idara hizo ni Utawala, Wakimbizi, Jeshi la Polisi, Uhamiaji,
Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Huduma kwa Wakimbizi.

Kikao hicho kilijadili mchakato wa ajira kwa watumishi wa
idara zilizopo chini ya Wizara hiyo, upandishaji vyeo, taratibu
za uteuzi na nidhamu katika vyombo vya ulinzi na usalama.

“Naipongeza Wizara kwa kuandaa mkutano huu ili kujadili
changamoto, mafanikio, idara ya utawala na rasilimali watu ina
jukumu kubwa zikishughulika na watu, watumishi.

“Pia idara hizi ndio kiungo katika uratibu, uwezeshaji kwenye
taasisi na vyombo vilivyopo chini ya Wizara ili kuleta mafanikio
zaidi kama watatekeleza wajibu wao ipasavyo,” alifafanua.

Meja Jenerali Kingu alisema idara hizo zina jukumu kubwa la
kuzishauri mamlaka ndani ya taasisi, vyombo husika kwani
kukiwa na tatizo ina maana kuna mahali hakuko sawa.
Alisisitiza suala la kutolewa mafunzo ya kitaaluma kwa
watumishi wote ambayo tatazingatia usawa.

“Suala la kuajiri watu kwa upendeleo lisipewe nafasi, tuajiri
watumishi wenye sifa kwa manufaa ya taasisi,” alisisitiza.

Alizungumzia suala la wastaafu kucheleweshewa malipo yao
akitaka wapunguziwe adha wanayoipata na kutaka yafanyike
maandalizi mapema ili kuondoa kero, kasoro zilizopo na
malalamiko ambayo si ya lazima.

Alisisitiza umuhimu wa kila mkuu wa idara kufuata sheria,
taratibu za utumishi wa umma hasa pale ambapo watumishi
wanapofanya makosa ili yasiweze kujirudia.

Akizungumzia majukumu ya viongozi hao, Meja Jenerali Kingu
aliwataka wasisubiri kukumbushwa wajibu wao, kila kiongozi
ayatambue majukumu aliyonayo na kuyatekeleza kwa ufanisi
yakiwemo ya wastaafu, nidhamu, uhamisho kwa watumishi.

Aliwataka wakuu wa idara kushirikiana na watumishi ili kuwe
na mpangilio mzuri wa kazi, kuongeza ufanisi na uwajibikaji.

“Naamini idara zote zilizopo chini ya Wizara hii zina watendaji
wazuri wanaojua wajibu wao na wachapakazi hivyo tuwatumie,
kuwepo na mpango mkakati wa kuondoa kero mbalimbali.

“Kero hizo ni pamoja na suala la kama mishahara, stahiki za
watumishi na upadishaji vyeo…utakuta mtumishi kapanda cheo
muda mrefu lakini anapata mshahara wa zamani usiolingana na
nafasi mpya aliyonayo, kuwepo mabadiliko,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimali Watu, Emanuel Kayuni, alimshukuru Meja Jenerali
Kingu kwa maagizo aliyotoa na kuahidi yatafanyiwa kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...