Na Khadija Seif, Michuzi TV
MSANII wa Bongofleva Ally Saleh a.k.a Alikiba atunukiwa cheti cha ubalozi wa utalii wa ndani na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
"Nina furaha kubwa kutunukiwa Cheti cha ubalozi wa Utalii wa ndani ili kuongeza chachu zaidi katika kukuza utalii wa Zanzibar na Tanzania kiujumla kwa Watanzania wenzangu na hata watalii kutoka nchi mbalimbali..." amesema Kiba.
Ali Kiba ametoa Shukrani za dhati kwa Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kwa kuona mchango wake utafaa katika hilo.
"Nazidi kuziomba serikali zetu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar ziendelee kuthamini mchango wa wasanii wa Tasnia mbalimbali na watutumie katika kukuza sekta mbalimbali katika Nchi yetu,"
Ali Kiba amekua akitumia baadhi ya vivutio vingi katika kutangaza utalii wa Tanzania Kama vile kutumia wanyama kama tembo na wengine kwenye Sanaa yake ya muziki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...