BENKI
ya Taifa ya Biashara (NBC), imetoa wito kwa wazazi kote nchini kufungua
akaunti maalumu ya watoto ya Chanua pamoja na bima ya elimu ya Educare
za benki hiyo ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao pindi wawapo hai
ama wasipokuwepo.
Wito
huo umetolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa
Wateja Binafsi wa benki hiyo, Benjamin Nkaka katika hafla waliyoiandaa
kwa ajili ya watoto wa wateja wao ikiwa ni sehemu ya matukio ya
kuadhimisha Mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.
Mkurugenzi
huyo alisema akaunti ya watoto ya Chanua ya NBC pamoja na bima ya elimu
ya educare vitamuwezesha mzazi kuanza kuwekeza kidogodogo kwa ajili ya
mtoto wake hivyo kuondoa hofu ya watoto kupata elimu bora pindi mzazi
anapoondoka duniani.
“Akaunti
ya Chanua na bima ya Educare za NBC ni suluhisho la uhakika kwa elimu
ya watoto, wakati mzazi awapo duniani,asipokuwepo au atakapotapa ulemavu
wa kudumu, nawashauri wazazi kuwafungulia watoto wenu akaunti hii na
kuanza kuwekeza pamoja na bima ya educare zote kutoka NBC,” alisema.
Kuhusu
hafla hiyo Bwana Nkaka alisema NBC imekuwa na desturi ya kukutana na
wateja wao mara kwa mara ikiwa ni moja ya azma yao ya kusogeza huduma
zao karibu na wateja wao hivyo licha ya kuwaeleza watoto walioambata na
wazazi wao bidhaa mbalimbali zinazotolewa na benki hususan
zinazowalenga watoto, lakini pia watoto walishiriki burudani za aina
mbalimbali jambo ambalo ni muhimu katika malezi ya watoto.
“NBC
imekuwa ikibadilika siku hadi siku tukitumia njia mbalimbali katika
kuwafikia wateja wetu, licha ya kuwa na mtandao mpana wa matawi lakini
pia tumeanzisha NBC Kiganjani inayomuwezesha mteja kupata huduma
mbalimbali za kibenki kwa kupitia simu yake ya mkononi.
“Lakini
hii haitoshi NBC inao mtandao mkubwa wa mawakala wake wakitoa huduma
mbalimbali za kibenki nchini kote, lakini hivi karibuni tumeingia
ushirika na Shirika la Posta ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma
zetu za kibenki katika ofisi zote za shirika hilo mahali kote nchini,”
aliongeza mkurugenzi hiuyo.
Ofisa Malipo ya Ndani wa NBC, Suzyo Gwebe
Nyirenda akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo katika
hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki
hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar
es Salaam hivi karibuni.
Meneja Huduma Bora wa NBC, Jane Dogani
akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo katika hafla ambayo
NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo
kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam jana.
Baadhi ya watoto waliohudhuria katika
hafla hiyo wakichorwa picha ikiwa ni sehemu ya shamra shamra zilizokuwepo
katika kuadhimisha moja ya matukio ya mwezi wa huduma kwa wateja ambapo NBC
iliandaa sherehe hiyo kwa watoto wa wateja wao. 
Baadhi ya watoto walihudhuria hafla hiyo
wakifurahia burudani mbalimbali zilizokuwepo katika siku hiyo ikiwa ni moja ya
matukio ya NBC kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja.
Meneja Huduma Bora wa NBC, Jane Dogani
akiwawekea chakula baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ambayo
NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo
kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa
benki ya NBC, Benjamin Nkaka akizungumza na watoto wa wateja wa benki hiyo pamoja
na wafanyakazi kuhusu umuhimu wa wazazi kuwafungulioa watoto wao akaunti ya
Chanua na pia bima ya elimu ya educare ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao
wakati wawapo hai ama wasipokuwepo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto
hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa
wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...