Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akikabidhi leseni ya uchimbaji madini kwa mmoja wa wachimbaji wa mgodi huo wa Suguta wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akizungumza na wachimbaji wa mgodi wa madini ya Sunstone wilayani humo baada ya kuyafungua na kuwakabidhi leseni ya uchimbaji.
MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deo Ndejembi amefungua mgodi wa madini ya Sunstone katika eneo la Suguta Kata ya Iduo wilayani humo ambayo aliyafunga miezi minne iliyopita baada ya kutokea kwa vifo vya wachimbaji wanne.
Akizungumza baada ya kufungua mgodi huo DC Ndejembi amewataka wachimbaji wa kikundi cha Hapa Kazi tu ambao ndio wachimbaji wa machimbo hayo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za madini.
DC Ndejembi amesema baada ya kujiridhisha kuwa hali ya usalama ni nzuri ameamua kuyafungua ili wachimbaji hao waendelee na kazi zao kama kawaida.
" Baada ya kujiridhisha kwa kushirikiana na Ofisi ya Madini Mkoa tumeamua tuyafungue machimbo haya ili muendelee na kazi zenu, niwasihi mtunze mazingira na ndio maana pia nimeambatana na Ofisi ya Mazingira ya Mkoa hapa. Fanyeni kazi kwa kufuata taratibu ambazo zimewekwa.
Ninafungua mgodi huu na nitawakabidhi pia leseni yenu ya kufanya kazi. Fanyeni kazi kama ambavyo jina lenu la Hapa Kazi linavyosema endeleeni pia kumuunga mkono Rais wetu na kama kukiwa na changamoto yoyote ofisi yangu ipo wazi njooni tushirikiane," Amesema DC Ndejembi.
Nae mmoja wa wachimbaji wa mgodi huo, John Joseph amemshukuru DC Ndejembi kwa kuwafungulia mgodi huo ambao ulifungwa na kumuahidi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu walizowekea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...