MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na CDF, Generali Venance MabeyoAmeongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa na Kukagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji. 

Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wametembelea mpaka wa Tanzania na Msumbiji kwa lengo la kuhakikisha mpaka huo na wananchi wa maeneo hayo wako salama, hatua hiyo imekuja baada ya kusemekana nchini Msumbiji kunavitendo vinavyoashilia Ugaidi vinaendelea nchini humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini CDF, General Venance Salvatory Mabeyo, huku akisisitiza kuwa kwa sasa mpaka uko salama na wakazi wa maeneo hayo wanatakiwa kuendelea na majukum yao ya kila siku.

Aidha kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema hali ya nchi kwa sasa ni salama na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuendelea kudumisha amani na usalama nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...