Mkufunzi
na Mkuu wa Idara ya Ufundi ya JKA/WF-‐Tanzania kitaifa, pia Mwenyekiti
wa Tanzania Shotokan-‐Ryu Karate-‐Do Association (TASHOKA) Abdallah
Kambi Sensei amefariki dunia.
Kambi
Sensei aliyeingia madarakani tarehe 27 Julai 2019, amefikwa na umautio
leo alfajiri katika hospital kuu ya Taifa Muhimbili, alipokua amelazwa
kufuatia kusumbuliwa na kifua na tumbo, tangu mwezi August.
Mwenyekiti,
JKA/WF-‐Tanzania Jerome G. Mhagama, amethibitisha kutokea kwa msiba
huo, na ameeleza taratibu za maziko ya Kambi Sensei aambaye alijiunga na
JKA/WF-‐Tanzania mwaka 2009 na kuwa mwanafamilia hai wa JKA mpaka
umauti unamkuta.
Katika
hatua nyingine Mhagama ameeleza taarifa nyingine za msiba wa mdau huyo
wa mchezo wa Karate, huku wakitarajia majibu wa kikao cha familia ya
marehemu.
Ndani
ya JKA Kambi Sensei alikuwa mmoja wa Wakufunzi tegemezi mwenye Black
Belt 4th Dan-‐JKA, pia alikuwa na JKA International Licence yenye
viwango vya Instructor class C, Judge class D & Examiner class
D.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Alale mahali pema peponi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...