Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na watu wenye
mahitaji maalumu,kuilia kwake ni Philipo Meli Mwenyekiti wa watu
wasioona mkoa wa Arusha ,kushoto kwake ni Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa
kanda ya ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA na wa kwanza
mulia ni Katibu wa chama cha Viziwi Tanzania tawi la Arusha .Picha na
Vero Ignatus.
MHANDISI
Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu
wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona
Julius Felix Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano
nchini kanda ya Kaskazini TCRA ,wengine ni washiriki wa semina hiyo ya
siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwaajili ya kuwajengea uelewa
juu ya usajili wa laini za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole.
Jan Kaaya ni Mhandisi Mwanadamizi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA).Picha na Vero Ignatus
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona
uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus
MHANDISI
Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu
wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona katika ukumbi wa
mkuu wa mkoa Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona
uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona
uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa kanda ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano
nchini TCRA akizungumza katika uzinduzi wa semina hiyo ya siku moja ya
wadau wa mawasiliano ,kutoka makundi mawili Viziwi na walemavu wa
kutoona.Picha na Vero Ignatus.
Mmmoja
wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu
kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wa siku moja ulioandaliwa
na TCRA Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Mmmoja
wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu
kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wasiku moja ulioandaliwa
na TCRA Mkoani Arusha.Pcha na Vero Ignatus
Baadhi
ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona
.Picha na Vero Ignatus.
Mmoja
wa wakalimani wa lugha ya aklama akisaidia ujumbe ufike kwa waandaaji
wa semina ya watu wenye mahitaji maalum (TCRA).Picha na Vero Ignatus
Na.Vero Ignatus,Arusha .
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kanda ya kaskazini
imefanya mkutano wa siku moja na wadau wa mawasiliano wenyenye mahitaji maalumu,
wakiwa katika makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutokuona.
Lengo haswa la mkutano huo ni kutoa uelewa kwa watu
wenye mahitaji maalum, kuhusu zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya
mfumo wa alama za vidole ,pia kuangalia changamoto mbalimbali walizonazo katika huduma
za Mawasiliano
Gabriel Daqqaro
ni mkuu wa wilaya ya Arusha amesema kuwa semina hiyo itasaidia ,ukizingatia kwasasa kuna changamoto nyingi
za mitandao japo kuwa zipo faida zake kama vile kupashana
habari,kuelimisha,kuburudisha na kukataza yale mambo mabaya katika jamii katika
maendeleo yanayokwenda kwa kasi.
Amesema kuna makosa ya uhalifu wa kimtandao ,watu
wasiowaaminifu wanaotuma jumbe za kulaghai wa wananchi,kwasababu hiyo serikali
imeelekeza laini zote za simu zisajiliwe
kwa alama za vidole ,hivyo ameipongeza TCRA kwa kuona watu wenye ulemavu kuwa
ni sehemu ya jamii.
“Watu hawa wenye mahitaji maalumu wananchwa mara
nyingine kutokana na baadhi ya watu kudhania kwa mawazo yao hasi kwamba ulemavu
ni hasara,niseme hujafa huijaumbika,nisisitize hebu tubebane tonane tupo sawa.
Daqqaro amesema serikali ya awamu ya tano imeona hilo, ndipo
ikaona watu wenye mahitaji maalum ,walikuwa hawajajumuishwa katika kunufaika na
zile 10% za mapato ya ndani ,kuanzia mwaka 2018 imetoa maelekezo kwamba na
wenyewe ni miongoni mwa kundi linalotakiwa kunufaika ,ambapo halmashauri zote zimeelekezwa hivyo .
Amesema ni muhimu kusajili line za simu ili kuepusha
makosa ya uhalifu wa kimtandao, matapeli wanao tuma jumbne
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina hiyo mkuu wa wilaya ya Arusha amesema serikali
serikali iliagiza kuwa 10%za mapato nao watu wenye ulemavu wanufaikike na
mapato ya ndani iliagiza laini zote za simu zisajiliwe kwa mfumo wa alama za
vidole hivyo watu wenye uhitaji maalumu nao ni sehemu ya jamii.
MHANDISI Imelda
Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini(TCRA) amesema kuwa Mamlaka hiyo
imeamua kwasababu wao nao ni sehemu ya jamii ,na pia wanatumia huduma ya
mawasiliano hivyo .wanahaki ya kupata taarifa mbalimbali,mafunzo.
“Tunafahamu
kwa namna walivyo wenzetu wana changamoto mbalimbali yumkini kuna wengine
hawawezi kupata taarifa kwa wakati ,lakini kwa wenzetu wa kwa wasiosikia
taarifa kwa taarifa zinazopelekwa kwa jamii kwa njia ya radio,televisheni,asiyeona hawezi kuona
kwenye televisheni,halikadhalika asiyesikia vileviel”
TCRA imesema kwa
kuona umuhimu wa kundi hilo wameamua kuwashirikisha Mamlaka ya vitambulisho vya
Taifa (NIDA)ili waweze kutoa huduma kwa watu hao wenye mahitaji maalum
Mkuu huyo wa
kanda ya amesema Swala la usiri na faragha kwa watu wasioona bado
limekuwa ni tatizo ,mawasiliano yao
yanaweza kutatuliwa tu endapo kuna vifaa maalumu ambavyo wanaweza kuvitumia
zikiwemo simu za mkononi ,pale mtu anaposoma ujumbe aweze kusikia sauti ujumbe
unasemaje.
''Ila mamlaka ya mawasiliano tunajitahidi kuona ni kwa
namna gani tunaweza kuwasaidia ,kwa wenzetu wasioona tunawapa taarifa
mbalimbali kupitia vitabu ambavyo vimechapiushwa kwa zile alama zao maalum.''
Ameainisha kuwa kila mmoja aone umuhimu wa kujisajili ni kwani watakaposajili
kutumia alama za vidole taarifa zao zinafahamika ,sambamba na kuimarusha usalama wanapotumia
mawasiliano.
Ametoa wito kwa jamii kulitilia uzito swala hili la
kusajili laini,na kwa wale ambao
hawajapata kitambulisho cha NIDA,Mamlaka husika itawasaidia kupata namba
zao,sambamba na wale ambao hawajajiandikisha NIDA wapo tayari kwaajili ya
kuwasaidi ili wajiandikishe wapate kitambuluisho cha taifa.
Philipo Meli
ni mwenyekiti wa wasioona mkoani Arusha amesema wanaishukuru TCRA kwa
kuwathamini na kuwapatia semina hiyo ya kuwajengea utaalamu na kuwapatia
vitabu vya nykta nundu kwaajili ya kujisomea na kupata uelewa kuhusiana
na mamlaka hiyo ya mawasiliano.
Amesema
katika mawasiliano watu wasioona changamoto kubwa ni mtu wa kuwasomea
ujumbe lazima awepo,hakuna usiri,tunaomba serikali itusaidie uwepo wa
simu ,ambazo tunaweza kusoma ujumbe kwa kusikia sauti ,na iwe katika
lugha ya kiswahili ambapo itaweza kuondoa utegemezi kwa kiwango kikubwa.
"Changamoto
kubwa mtu anakutumia ujumbe hata kama unataka uwe wa siri,inashindikana
mpaka utafute mtu mwaninifu aweze kukusomea ujumbe wako,hiyo ndiyo
changamoto inayotupata sisi watu tusioona.''Alisema Philipo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...