Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Benki ya TIB Corpotare wamekata keki na kusherehekea kwa pamoja na wateja wao katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Hayo yamefanyika leo katika matawi tofauti ya benki hiyo yaliyopo Jijini Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.
Akizungumza baada ya kumaliza kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja,Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Corporate Theresia Soka amesema kwa mwaka huu wameleta huduma ya JIPANGE inayomwezesha mteja kuweka akiba na kujipatia faida.
Amesema, mbali na hilo jukumu lao ni kuona wateja wao wanapata huduma bora za kibenki na sio bora katika mlengo mbalimbali.
Theresia amesema, huduma ya JIPANGE inamuhusu mzazi, mtoto, Kijana, Mzee na hata kama kampuni inayotoa huduma kwa jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...