Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa kwa siku mbili.

Angalizo hilo limetolewa kwa leo, Oktoba 16, 2019 na kutaja maeneo yatakayokumbwa na mvua hiyo kuwa ni mikoa ya Kagera,Geita,Mwanza,Kigoma, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa kutoka TMA zimesema mvua hizo zitaanza kunyesha kesho Oktoba 19 hadi Oktoba 20, 2019 hivyo wakazi wa mikoa tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.

Kwa sababu hiyo athari zitakazotokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...