Mwenyekiti wa Chama cha Madalali Wanaosafirisha Mizigo Tanzania, Rajabu Masasi akizungumzia malengo yao kwa Wamiliki wa Malori nchini.
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
CHAMA Mwenyekiti wa TAMSTOA, Chuki Shaaban (TAMSTOA) kimeeleza kufika mwafaka na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuhusu Magari hayo yanayosafirisha mizigo nje ya nchi ili kuondoa vikwazo katika usafirishaji nje ya nchi.
Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo kati ya Uongozi wa Chama hicho na Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Abdul Mapembe kwa Madereva wa Malori hawatakamatwa tena kwa ajili ya Mashine ya EFD lakini madereva hao wanapaswa kuwa na Risiti ya Mashine hiyo ya EFD ili kupata Leseni mpya ya usafirishaji mizigo nje ya nchi ifikapo 2020.
Mwenyekiti wa TAMSTOA, Chuki Shaaban amethibitisha kufika makubaliano hayo, amesema wamekubaliana na TRA, ili kupata leseni ya sasa ya usafirishaji mizigo Nje ya Nchi kwa Dereva lazima awe na Risiti ya yakununulia Mashine ya EFD ili kuondoa vikwazo katika usafirishaji mizigo.
''Wenzetu wanaotoka Nje ya Nchi wanaotumia Bandari yetu wanalalamika mzigo haifiki kwa wakati kwa sababu ya mambo yetu ya ndani, kwa hiyo Kamishna akasema tukutane, tujadili sual hilo''; amesema Chuki.
Pia amesema TAMSTOA imepunguza ada ya kupata Cheti, amesema wamebaini Wanachama wao wanashindwa kutatua changamoto zao kutokana hawana anuani kamili ya Chama hicho kupata taarifa. Chuki amesema ili kupata cheti katika Chama hicho lazima uwe na Kitambulisho cha Mmiliki wa Lori, Picha ya Mmili, Anuani (Address) na taarifa zozote za mawasiliano.
Nao Chama cha Madalali Wanaosafirisha Mizigo Tanzania, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Rajabu Masasi amesema chngamoto walizokuwa nazo kwenye udalali tayari wamezijadili kwa kina, wana lengo lakuwaweka Wamiliki kuwa sehemu salama, amasema wamejadiliana kuwa na ushirikiano na Wamiliki wa Malori.
Mmoja wa Dereva wa Malori, Said Mascat ameishukuru Serikali kupunguza kero, changamoto nyingi kwa Madereva kwa kiasi kikubwa, amempongeza Rais Magufuli katika utawala wake kutokana na haki inayotendeka wanapokuwa katika majukumu yao ya udereva.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...