
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Seif Ali Idd (wa tatu kutoka kulia), akiwa amenyanyua juu picha maalum yenye muonekano wa Gazeti la Uhuru ya Kijani mara baada ya kuzinduliwa mbele ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na Viongozi mbali mbali wa CCM huko Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Seif Ali Idd, na Viongozi mbali mbali wa CCM wakionyesha Magazeti ya Uhuru wa Kijani mara baada ya kuzinduliwa kwa upande wa Zanzibar, yanayomilikiwa na kampuni ya Uhuru Media Group (UMG).
BAADHI ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walioudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Toleo jipya la Uhuru ya Kijani kinalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group,lililozinduliwa rasmi na Mjumbe wa Kamati Kuu Balozi Seif Ali Idd kwa upande wa Zanzibar.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...