WADAU wa Sayansi, Technolojia na Wabunifu 250 kukutana pamoja katika mkutano wa viongozi wa kikanda wa baraza la Sayansi kanda ya Afrika ulioandaliwa na Tume ya Sayansi na technolojia nchini, COSTECH.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Kaimu Meneja wa Utafiti wa Sayansi hai wa COSTECH, Dk. Hulda Gideon, amesema kuwa mkutano wa viongozi wa baraza la Sayansi kanda ya Afrika unatarajia kufanyika Novemba 11 hadi 15, 2019, jijini Dar es Salalaam katika hoteli ya Serena Novemba 11 hadi 15, 2019.
"Mkutano huu utahusisha wadau wa Sayansi, Technolojia na Ubunifu pamoja na wanasayansi, wafadhili, watunga sera washirika wa Maendeleo pamoja na wanahabari". Amesema Hulda.
Mada kuu katika mkutano huo ni Uwazi wa Sayansi kwa Maendeleo endelevu na ushirika wa umma katika masuala ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu.
Hata hivyo Mkutano huo wa viongozi wa kikanda utaambatana na maonesho ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU).
Dk. Hulda amesema kuwa Mada zitkazotolewa katika mkutano huo zitaaaidia kutayarisha ajenda za mkutano wa baraza la dunia utakaofanyika Afrika ya kusini 2020.
Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Amos Nungu amewaomba wadau wa STI na umma kwa Ujumla kuyambua uwepo wa mkutano huo wa viongozi wa juu wa Sayansi wa Afrika.
Nungu amesema kuwa Mkutano huo utafunguliwa rasmi na waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako Novemba 11 jioni katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar ea Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya sayansi na Teknolojia, Dk. Amosi Nungu akizungumza na waandishi wa haabri jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Profesa Mohammed Sheikh.
Kaimu Meneja wa Utafiti wa Sayansi Hai wa COSTECH, Hulda Gideon akizungumza na waandiahi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akielezea kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa Kanda ya Afrika wa Sayansi. Mkutano huo utafanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam, Paul Onyango (Mwenye shati lenye Draft) akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...