Na
Leandra Gabriel, Michuzi Tv
KWA
mujibu ya mtandao wa Worldometers
unaofuatilia matukio yanayotokea duniani kwa kila sekunde, leo Oktoba 18 idadi
ya watu nchini India imefikia 1,370,455,147 kwa mujibu wa data za umoja wa
Mataifa.
Kwa
mujibu wa wa data za mwaka 2018, China nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi
zaidi duniani iliizidi India kwa zaidi ya watu milioni 41 na kufanya nchi hizo mbili kubeba asilimia 36.28 ya idadi
ya watu 7,632,819,325 duniani kote kwa mwaka 2018.
Licha
ya India kuwa na watu wengi zaidi bado imeendelea kutunza na kuhifadhi Miji na
maeneo mbalimbali ambayo hutembelewa na watalii, kwa mujibu wa jarida la
Culture Trip la India Miji maarufu na yenye kuvutia zaidi nchini humo ni pamoja
na ;
Jaipur
Mji
huu hujulikana zaidi kama “Pink City”na hiyo ni kutokana na majengo yake
kupakwa rangi ya Pinki mwaka 1976 wakati wakimkaribisha Malkia Victoria na
mwana mfalme wa Wales.
Pembe
tatu ya dhahabu na mahekalu huwavutia maelfu ya Wahindi na watalii kutoka nje
ya nchi kila mwaka.
Veranasi
Umaarufu
wa Mji huu ni kubeba historia ya kiimani huko Kaskazini mwa India, historia
yake ilianza karne ya 11 baada ya Kristo na inaelezwa kuwa hii ni sehemu kongwe
zaidi duniani. Mji huu umebeba mahekalu mbalimbali, makuhani, wajasiriamali na
makazi ya watu.
Udaipur
Mji
huu ni maarufu zaidi kwa maziwa (Lakes,) ngome, makanisa pamoja na majumba ya
kifalme, unapatikana Rajasthan na hupendelewa zaidi na wapendanao kutokana na
bustani nzuri za kuvutia zipatikanazo pia filamu nyingi zimechezwa Udaipur
ikiwemo ya James Bond- Octopussy (1983) pia sherehe mbalimbali hufanyika katika
Mji huo.
Bangalore
Umaarufu
wa Mji huu hutokana na uwepo wa viwanda vingi vya teknolojia ya kompyuta, na
hujulikana zaidi kama ‘Silicon Valley’pia Mji wenye misitu ya kijani inayowatia
wengi na umeendelea katika masuala ya taaluma.
Delhi
Ni
Mji mkuu wa nchi na Serikali, licha ya kufahamika hivyo Delhi imebeba tamaduni
na shughuli zake ikiwemo michoro na sanaa mbalimbali, sehemu nyingi za kupata
chakula kwa wageni hupatikana Delhi na hiyo ni pamoja na kuwepo kwa makanisa,
misikiti, na ngome maarufu zaidi zikiwemo Red Fort, Jama Masjid na ngome ya
Baha’i Lotus.
Chennai
Ni
Mji wa kiutamaduni, michoro ya utamaduni na huwavutia wageni wengi zaidi na ni
maarufu zaidi kwa watalii.
Mysore
Unapatikana
Kusini mwa India, na ni moja kati Mji uliopangwa vizuri nchini humo, Mji wa pili kwa usafi India huku ukiwa mji wa
tamaduni zaidi huko Karnataka. Pia Mji huu ni maarufu kwa mchezo wa Yoga (
Ashtanga Yoga ilianzia hapa.)
Agra
Mji
huu ni sehemu ya maajabu saba ya dunia, umaarufu wa Agra ni kutokana na sehemu
mbili za urithi wa shirika Umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya Agra Fort na Fatehpur Sikri.
Kolkata
Ni
Mji wa utamaduni ambao watu maarufu wakiwemo waimbaji, waigizaji, waandishi,
washindi wa tuzo za Nobel na watayarishaji wa filamu wanaishi. Pia Mji huo una
hazina ya vyuo vya utalii na bustani nyingi za maua.
Mumbai
Mji
huu ulianza mwaka 1911, upo pembezoni mwa bahari na hapo awali ulijulikana kama
Bombay, ni kitovu cha uchumi pamoja na vivutio vya utalii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...