Rais wa PCI, Carrie Hetessler-Radelet,akizungumzia juu ya mradi huo ambao wafugaji watatumia simu za mkononi kufahamu maeneo ya malisho na maji.



Na.Vero Ignatus,Monduli

Simu za mkononi zitatumika kutuma jumbe kuulizia eneo lenye maji,malisho katika wilaya tatu za mkoa wa Arusha 

Mradi huu umezinduliwa na shirika la kimataifa la PCI ,l, katika kijiji cha Arkaria wilayani Monduli na utatekelezwa pia wilaya za Longido na Ngorongoro ambazo zina idadi kubwa ya mifugo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais wa PCI, Carrie Hetessler-Radelet alisema, wafugaji kupitia simu zao za mkononi, baada yakupakuwa application ya Afriscout watatuma bure ujumbe kwenda15054 kuuliza malisho na maji.

Hetessler –Radalet amesema baada ya kuuliza,mtandao huo utaonesha ramani za sehemu ya maji na malisho ambayo imepigwa angani.

Amesema mradi huo, utawezesha wafugaji kuacha kusafiri muda mrefu kusaka malisho, kuharibu mazingira lakini pia utapunguza vifo vya mifugo na adha ya wafugaji kushindwa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Jennifer Waungaman amesema mradi huo ambao unatarajiwa kuwanufaisha sana wafugaji.“Tunawaomba wafugaji kutumia huduma hii ambayo pia itawasaidia kusimamia vizuri nyanda za malisho yao”alisema Jennifer

Dkt.Asimwe Rwiguza ni Kaimu mkurugenzi endeshaji wa malisho na vyakula vya mifugo,katika uzinduzi huo alisema mradi ho una manufaa makubwa kwa wafugaji na amelitaka shirika hilo kupanua huduma hiyo nchi nzima.

Mfugaji John Laizer amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwao na itaondoa tatizo la mifugo kufariki wakati wa kiangazi na migogoro na wakulima.John Rutabingwa ni Mkurugenzi halmashauri ya Monduli, alisema halmashauri hiyo itaupa ushirikiano mradi huo ili wafugaji wanufaike zaidi.

Mradi huu pia unatekelezwa katika nchi tatu barani ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia na shirika hilo linafanya kazi katika nchi 16 Duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...