Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini(DCEA) imetekeleza dawa za kulevya kilo 120.91 za Heroine na kilo 70.96 za Cocaine zinazohusisha kesi 35.
Aidha uzito wa dawa hizo unajumuisha kilo 63.155 za Heroine ambazo kesi yake imehukumiwa mkoani Mtwara ikimhusisha Mwinyi Rajab na Ally Hamad na kushindwa kutekelezwa mkoani humo.
Utekelezaji wa dawa hizo umefanyika leo Oktoba 8,2019 katika kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam ambapo Mamlaka imefanya uteketezaji huo wa dawa za kulevya kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa ,Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Baraza la Taifa la Mazingira.
Kwa mujibu wa Mamlaka hiyo wakati wa kuteketezwa dawa hizo imeeleza kuwa dawa hizo zimehusiana na kesi zilizomalizika katika Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mkoani Dar es Salaam na kwamba jumla ya dawa za kulevya zilzoteketezwa ni kilo 120.91 au gramu 120.919.88 za heroine na kilo 70.96 (gramu 70.967.86) za Cocaine ambazo zinahusisha kesi 35.
"Hii ni mara ya kwanza uteketezaji dawa za kulevya kufanyika tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2919 kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mara ya mwisho uteketezaji kama huu ulifanyika mwaka 2015 katika kiwanda cha Wazo Hill ukihusisha dawa za kulevya za aina mbalimbali.
"Kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ili dawa za kulevya ziteketezwe lazima kuwepo a amri ya Mahakama iliyosikiliza kesi na kumalizia au ambapo kesi hiyo ipo.
"Pia uteketezaji wa dawa za kulevya hufanyika kwa utaratibu maalum ili kuepuka uharibifu wa mazingira na madhara ya kiafya kwa wananchi,hivyo viwanda vya saruji kutumika,"imesema Mamlaka hiyo kupitia Kitengo chake cha Habari na Mawasiliano.
Hata hivyo Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya umetoa rai kwa wananchi kutoa taarifa za wazalishaji, wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya ili sheria ichukue mkondo wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...