Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
ASKARI Polisi Itialy Omary na mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Lezilie Koini na wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kupokea rushwa ya Sh. 200,000/-
Hata hivyo mahakama imemsomea mashtaka mshtakiwa Koini peke yake kwani mshtakiwa Omary hajafika mahakamani hivyo mahakama imetoa amri ya kukamatwa kwake.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Odessa Horombe amedai Mei 8, 2018 mshtakiwa Omary na Koini kwa pamoja walipokea rushwa ya Sh. 200,000 kutoka kwa Mussa Abdallah ikiwa kama kishawishi ili asikutwe na we na hatia katika kosa namba 211/2018 la usalama barabarani.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa Omary alikubali kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai bado haujajiandaa hivyo wanaomba ahirisho la muda kwa ajili ya kujiandaa.
Hata hivyo Hakimu Mmbando alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa ambapo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na vitambulisho halali atakayesaini bondi ya Sh. 500,000.
Mshtakiwa ametimiza masharti ya dhamana, nje kwa dhamana, kesi itatajwa tena Novemba 21 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...