Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

ASKARI Polisi Itialy Omary na mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Lezilie Koini wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. 200,000.

Hata hivyo mahakama imemsomea mashtaka mshtakiwa Koini peke yake kwa kuwa mshtakiwa Omary hajafika mahakamani, hivyo Mahakama imetoa amri ya kukamatwa kwake.

Akizungumza leo Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Odessa Horombe amedai Mei 8, mwaka 2018 mshtakiwa Omary na Koini kwa pamoja walipokea rushwa ya Sh. 200,000 kutoka kwa Mussa Abdallah ikiwa kama kishawishi ili asikutwe na we na hatia katika kosa namba 211/2018 la usalama barabarani.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa Omary alikubali kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai bado haujajiandaa hivyo wanaomba ahirisho la muda kwa ajili ya kujiandaa. 

Hata hivyo, Hakimu Mmbando alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa ambapo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na vitambulisho halali atakayesaini bondi ya Sh. 500,000. 

Mshtakiwa ametimiza masharti ya dhamana, nje kwa dhamana.Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 21 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...