Benki ya NBC Yatangaza kupata ongezeko la faida kwa asilimia 300

Dar es Salaam, 3 Novemba, 2019: BENKI ya NBC imeonyesha ufanisi mkubwa katika utendaji wake baada ya kutangaza kupata ongezeko la faida (baada ya kodi) la asilimia 367 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mafanikio hayo yanatajwa kusababishwa na ufanisi wa benki hiyo katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika usimamizi wa mizania, kuongezeka kwa mapato yatokanayo na ada ya mihamala na kuboreshwa kwa huduma za mikopo, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Theobald Sabi.

Kwa mujibu wa ripoti yake ya kifedha ya robo ya tatu ya mwaka 2019 iliyotolewa hivi karibuni, hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu, benki hiyo ilikuwa na jumla mikopo yenye thamani ya TSh 987 bilioni huku ikiwa na amana za wateja zenye thamani ya Tsh 1.717 Trilioni

"Jumla kuu ya Mikopo yetu imeongezeka katika kipindi cha robo mwaka kwa asilimia 3.7, hasa ikichangiwa na ongezeko la uombaji wa mikopo kutoka kwa wateja wetu wakubwa, wa reja reja na wa kati huku amana zetu (customer deposits) kwa ujumla ziliongezeka kwa asilimia 19.3" Aliongeza Bw Sabi.

"Umakini na ufanisi wetu katika suala zima la utoaji wa mikopo limeanza kutupa faida kwa kuwa hata kiwango cha mikopo chechefu kimeendelea kupungua hadi kufikia asilimia 6.9 kutoka asilimia 10.1 katika kipindi kama hiki mwaka uliopita,’’ alibainisha Bw Sabi.

Aliongeza kuwa mkakati wa mabadiliko ya kidigitali unaotekelezwa na benki hiyo umeendelea kuzaa matunda ya ukuaji huo huku akibainisha kuwa mfumo wa miamala kwa njia ya simu umekua kwa asilimia 50 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

“Ongezeko hili ni ishara kwamba wateja wetu wanapokea vizuri mabadiliko ya uboreshaji wa huduma zetu hasa kidigitali na hivyo kutupunguzia kiasi cha muda ambao tungeutumia kuwahudumia kupitia matawi yetu na hivyo tunajikuta tunapata muda wa kutosha kubuni na kutekeleza huduma nyingine bora zaidi kwa ajili yao,’’ alisema.

Alihamasisha zaidi wateja wa benki hiyo wakiwemo wa reja reja na wateja wakubwa yakiwemo mashirika na taasisisi (corporates)kuendelea kutumia huduma hizo za kidigitali kwa kuwa ni salama na zinatoa huduma ya malipo ya ya aina zote yakiwemo malipo makubwa kwa ndani na nje ya nchi.

Aidha Bw Sabi aliitaja huduma nyingine ya kielectronic inayokua kwa kasi kuwa ni NBC Wakala ambayo kwasasa ina mtandao wa mawakala zaidi ya 2,000 waliotapakaa nchi nzima.

“Wateja sasa wana uwezo wa kuzifikia akaunti zao na hufanya mihamala kwa urahisi zaidi kupitia maelfu haya ya mawakala nchi nzima.’’

“Mawakala wa NBC kwasasa wamefuzu kufanya mihamala kupitia mfumo wa kielectronic wa malipo serikalini (GePG) na hivyo wateja wanaweza kuwatumia kufanya malipo yao kwenye taasisi na mashirika ya serikali na ndio sababu Benki ya NBC sasa ni moja wapo ya benki inayoongoza kwa Makusanyo ya Mapato ya Serikali kupitia GePG.’’Alisema. 


 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw  Theobald Sabi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...