Mkurugenzi
mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume, amewaasa
wanafunzi wa shule ya sekondari Loyola kujifunza kwa kuzingatia mtizamo
mpana wa kidunia ili kuendana na mfumo wa sasa wa kielimu wa kidunia
unaohitaji wahitimu wenye uwezo mkubwa wa kuelewa mambo na matatizo
mbali mbali na kisha kuyatafutia suluhisho.
Karume
aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 21 ya shule hiyo alitoa wito
huo, sambamba na kukabidhi mchango wa magodoro 100 kwa ajili ya
kuboresha mazingira wanayoishi wanafunzi wa shule hiyo.
Mkurugenzi
huyo pia aliwaambia wanafuzi wa Loyola kuwa ili kuendana na dunia ya
sasa, wanatakiwa kufanya jitihada binafsi za kutafuta maarifa na ujuzi
na siyo tu kutegemea kile wanachofundishwa na waalimu wao darasani na kusisitiza kuwa bado wana safari ndefu.
“Elimu
mliyoipata bado ni ya hatua za mwanzo tu, hasa ukizingatia kukua kwa
utandawazi. Kutokana na mabadiliko makubwa yanayoenda sambamba na ukuaji
wa haraka wa Sayansi na Teknalojia yanayomgusa kila mtu na katika kila
nyanja ya maisha, sote tutalazimika kuendelea form 6 kujifunza mambo
mapya hadi mwisho wa maisha yetu,” alisema
Karume
aliwaambia wahitimu hao watarajiwa kwamba ni wajibu wao kuendelea
kujifunza mbinu mpya za kuyakabiliana na maisha na pia kujijengea uwezo
wa kujiajiri pindi watakapomaliza elimu ya juu
Elimu
mliyopata na ambayo mtaendelea kuipata itafungua maisha yenu na ya
jamii nzima ikiwa ni pamoja na familia zenu na watoto wenu. Elimu hii
pia itawapa uwezo wa kiuchumi, itawapa uwezo wa kuwa na sauti, mtaongea,
mtasikika na kusikilizwa, pia itawajengea heshima katika jamii na
kuwapa uwezo wa kuchangia mambo mbali mbali katika maisha.
Aliwataka
kuiga mifano ya wanafunzi waliosoma shuleni hapo na ambao wamefanikiwa
kimaisha baadhi yao wakiwa ndani na wengine nje ya nchi
Kwa
upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Padri Obwanda Meyo, SJ
alimuhakikishia mgeni rasmi kuwa wanafunzi wake wamejiandaa vizuri kwa
ajiili ya mitihani ya mwisho na hivyo watafanya vizuri
Mkurugenzi
mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (kushoto)
akiwa ni mgeni rasmi wa sherehe ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule
ya sekondari Loyola akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni
4.7/- kwa mkuu wa shule hiyo Father Ubwanda Meyo jana, ikiwa ni sehemu
ya mchango wa benki ya NIC kwa ajili ya kununulia magodoro 100
yatakayotumika kwenye mabweni ya wasichana wa shule hiyo.
Mkurugenzi
mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume akizungumza
na wageni waalikwa , wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Loyola
waliohudhuria kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne shule hiyo
jana jijini Dar es salaam
Mkurugenzi
mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (wa pili
kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa shule ya sekondari
Loyola, Padri Obwanda Meyo (wa tatu kulia), mwakilishi wa wazazi watoto
wa kidato cha nne, Joseph Tadayo (kulia), Brigitte Asenga na Annah
Lupembe (kushoto) ambaye ni meneja wa tawi la NIC Kariakoo.
Mkurugenzi
mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume akifurahi na
wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Loyola.
Mkurugenzi
mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (wa pili
kulia mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne
wa shule ya sekondari Loyola, Mkuu wa Shule Padri Obwanda (aliyebeba
mtoto), Mwakilishi wa wazazi, Joseph Tadayo , Mwenyekiti wa PTA Luyola,
Brigitte Asenge na Meneja wa Tawi la NIC Kariakoo, Annah Lupembe (mwisho
kushoto)
Mkurugenzi
mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume akiwa na
kikombe alichopewa zawadi na uongozi wa shule ya sekondari Loyola.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...