Bw. Jianpo Zhang akiwa na mkewe Shamsa Shaban Zhang wakiwa katika hafla hiyo wakifurahia pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
Bw. Jianpo Zhang akiwa na mkewe Shamsa Shaban Zhang wakiwa katika hafla hiyo wakifurahia pamoja na wageni waalikwa mbalimbali wakipata burudani ya muziki.
Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo ya kuwapongeza.

……………………………………………

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

MWANAFUNZI wa Chuo cha Mzumbe ambaye ni raia kutoka China Jianpo Zhang amesema anajisikia fahari kuoa Tanzania akidai kufanya hivyo mbali na kudumisha undugu baina ya familia hizo pia kunazidi kuboresha Uhusiano wa nchi za Tanzania na China.

Katika kuthibitisha kwa vitendo furaha aliyonayo Raia huyo wa China amefanya sherehe kubwa ya tunashukuru Watanzania na hasa wote ambao wameshiriki kikamilifu katika kufanikisha ndoa yake na mkewe Shamsa Shaban Zahng iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi mstaafu Robert Mboma.

Akizungumza wakati akitoa shukrani hizo Zhang amesema anajivunia kuoa mtanzania huyo akisisitiza kuwa binadamu wote ni ndugu na kitendo chake cha kufunga ndoa hiyo kitazidi kumfanya ajisikie kuwa kama yupo nyumbani huku akiwataka watanzania kuona fahari pia kwenda kuoa raia kutoka China.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu aliyoishi hapa nchini ameona mambo mengi mazuri na  kiasi cha kumfanya ajihisi yupo ‘nyumbani’  na zaidi akidai kuwa amani na upendo kutoka kwa watanzani ndiyo hasa jambo linalozidi kumuongezea hamasa ya kuona undugu unazidi kukua baina ya mataifa yote mawili.

Ameongeza kuwa furaha kwake Tanzania inazidi kukua kimaendeleo siku hadi siku chini ya uongozi wa Rais John Magufuli  ambaye pia anasema katika utawala wake ameona wazi wazi ushirikiano baina ya Tanzania na China ukizidi kuhimarika.

“Naipenda Tanzania, nawapenda watu wake na zaidi Rais John Magufuli ambaye katika utawala wake naona mambo mengi mazuri ukiwemo ujenzi wa miradi mbalimbali ikifanyika katika kiwango cha hali ya juu” alisema Zhang.

 Amesema mipango yake ya baadae ni kufanya biashara mbalimbali zinazoakisi mahitaji  uhimu ya kijamii ili ziweze kuzidi kumuweka karibu na watanzania anaodai kuwa kwa sasa ni ndugu zake hasa baada ya kumuoa mtanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...