Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii
WATAALAMU na wafanya maamuzi wa miradi mbalimbali nchini Tanzania wameshauriwa kuweka mgawanyo sawa katika maeneo yenye uhitaji wa miradi ikiwemo ya mabadiliko ya tabianchi na kuongeza rasilimari ili kuweza kupunguza kasi ya uhitaji.
Akizungumza Dar es Salaam leo Novemba 28,mwaka 2019 katika mkutano wa wadau wa masuala ya Mabadiliko ya tabianchi chini ya Mradi wa Uwajibikaji katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi (ACATI) unaofadhilia na Umoja wa Ulaya ,Mkurugenzi wa Shirika la ForumCC,Rebecca Muna amesema dhana ya uwajibikaji katika mambo ya mabadiliko ya tabianchi yanapaswa kuangalia kwa namna gani rasilimari zinaelekezwa mahali ambapo kuna uhitaji zaidi katika jamii inayoathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi.
Muna ameongeza wataalamu hao wanaopanga miradi iende wapi wanapaswa kuzingatia mahali ambapo kuna uhitaji zaidi na kuwa wawazi kuliko kuvutia miradi hiyo kupeleka katika maeneo yenye watu maarufu na wenye nguvu ya kuvuta rasilimali.
"Katika suala la uwajibikaji wa mabadiliko ya tabianchi yanapaswa kuangalia ni maeneo yapi yanapata changamoto hiyo na miradi inawafikia walengwa ipasavyo bila kubaguliwa.Kunahitajika kufanya ushawishi na utetezi kwa Serikali kuhakikisha katika bajeti zinaelekezwa katika vipaumbele vya uhimili wa mabadiliko ya tabianchi na kuangalia ni rasilimari zinawafikia watu walioathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi,"amesema.
Ameongeza ni wakati muafaka kuondoa mambo ya kupeleka miradi katika eneo moja bali ihakikishe inaangalia wapi kuna uhitaji zaidi ya uhimili wa mabadiliko ya tabianchi ili kupunguza uongezwaji wa athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo ambayo yameathirika zaidi.
Wakati huo Ofisa Mazingira na Mratibu wa Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini(NEMC),Fredrick Mulinda amefafanua baraza hilo ndilo linaosimamia mazingira na ni taasisi ilipochini ya Ofisi ya Makamu wa Rais na ndio yenye dhamana ya kuratibu masuala ya mabadiliko ya tabianchi Tanzania.
"Baraza hili linawakilisha nchi kama taasisi iliyopewa dhamana ya kupokea fedha za kuhimili mabadiliko ya tabianchi kutoka Mfuko wa Dunia wa Kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa nchi zinazoendelea.Baada ya kukamilisha kwa michakato mwaka 2017 kwa nchi zinazoendelea zinapata fursa ya kupata fedha Dola Milioni10 katika kutekeleza miradi iliyoathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi kwenye nchi husika,"amesema.
Ameongeza kwamba Serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais tayari imetekeleza mradi mmoja kwa moja ya shirika ambalo iligharimu Sh. Dola million tano na tayari kumefanyika mchakato wa kuandika miradi kwa baadhi ya taasisi za mabadiliko ya tabianchi ambapo takribani taasisi nne zimepita na zipo katika mchakato wa mwisho wa kupewa fedha hizo na kutekeleza miradi.
Kwa mujibu wa Mulinda amesema fedha hizo zinawafikia wananchi moja kwa moja katika kutelezewa miradi ya mabadiliko ya tabianchi katika maeneo husika ambapo kunaathari kubwa ya mabadiliko hayo na athari zinaonekama.
Wadau wa mabadiliko ya tabianchi wakiwa katika majadiliano kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na hatua zinazostahili kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko hayo. Wadau hao wamekutana chini ya Mradi wa Uwajibikaji katika Mabadiliko ya Tabianchi(ACATI) kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya
Mmoja wa wadau akitoa mada katika kikao cha majadiliano kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na hatua zinazostahili kuchukuliwa .Wadau wao wamekutana chini ya Mradi wa Uwajibikaji katika Mabadiliko ya Tabianchi(ACATI) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya
Wadau wa mabadiliko ya tabianchi wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu mabadiliko ya tabianchi chini Mradi wa Uwajibikaji katika Mabadiliko ya Tabianchi(ACATI)unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...