Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii-Dodoma

BODI ya Nyama Tanzania imekutana na wadau mbalimbali wanajihusisha na biashara ya nyama katika Mji wa Dodoma ambapo imewakumbusha hatua mbalimbali zinapaswa kufuata kwa watoa huduma hiyo ikiwa pamoja na kiheshimu sheria huku ikitangaza kuanza kuwasajili wadau wote.

Wamekumbushwa umuhimu wa mnyama kupumzishwa kati ya saa 12 hadi saa 24 kabla ya kuchinjwa ikiwa ni sehemu ya kumpunguzia mnyama mawazo huku wakikumbushwa nyama ubora wa nyama kwa uthibitisho wa daktari. 

Akizungumza leo Novemba 24 mwaka 2019 Mjini Dodoma Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama nchini Imani Paulo Sichalwe amewaaambia wanaojihusisha na biashara hiyo kuifanya kwa mujibu wa taratibu kwa kuafuata sheria na sio mazoea.

" Bodi ya Nyama leo tumeamua kukutana nanyi ili kutoa elimu kwa wadau wote wa nyama Dodoma kuhusu namna bora ya ubebaji nyama na taratibu za ufanyaji biashara ya nyama.Tunayo majukumu mengi na baadhi ya majukumu hayo ni kusimamia biashara ya nyama nchini kwa kuhakikisha sheria zote zinafuatwa, kwa ujumla ni kusimamia taratibu zote na watakaokiuka kuna adhabu zake ingawa huko kwenye adhabu sio mara nyingi .

"Ni mara ya kwanza kukutana na wadau wa sekta hiyo ya ufanyaji wa biashara ya nyama katika Jiji la Dodoma kwa wingi namna hii. Kazi ya tatu ni kuendeleza tasnia ya nyama ikiwa pamoja na kutoa elimu ambayo itawawezesha wadau kuwa na nyama iliyokidhi viwango,"amesema na kuongeza kuwa lengo la bodi ya nyama kuwepo na wadau hao ni kuzungumza na wadau hao na kukumbusha.

Sichwale amesema kuwa kwa hiyo wanatoa elimu hiyo kama sehemu ya kuakumbusha yanayotakiwa kufanywa na wadau wa nyama na kutambua mnyonyoro wote kuanzia nyama inapoanzia hadi inakwenda kwa mlaji.

Akizungumzia usafirishaji mnyama amesema ni muhimu kuzingatiwa kwa sheria ya mnyama kwani anayo sheria inayomlinda na anahaki zake na kwamba mnyama hatakiwi kuumizwa kwa kupigwa fimbo na anaposafirishwa mnyama lazima apumzike kila baada ya kilometa 300.Mnyama anaposafirishwa biashara nyama yake inakuwa sio nzuri na matokeo yake huonekana mwishoni.

Ameongeza kuwa pia wanyama nao wana mawazo na yanatokana na sababu mbalimbali ,kwani kuna wanyama ambao hawajawahi kuona gari wala kupandisha,hivyo huwa na mawazo."Tunashauri mnyama hatakiwi kupigwa kwani kunaharibu nyama kwani inakuwa ngumu kuihifadhi.Pia mnyama anapopigwa nyama inakuwa ngumu."

Kuhusu kuchinja nako kuna hatua zake ambazo lazima zifuatwe na kutoa mfano mnyama ambaye ni mgonjwa au amekonda sana hatakiwi kuchinjwa na kwamba katika kukidhi hatua hizo kuna wataalaam wakiwamo madaktari ambao kazi yao ni kuangalia ubora wa mnyama na nyama yenyewe."Mnyama kabla ya kuchinjwa anatakiwa kumpumzika kati ya saa 12 na saa 24 .Kumpumzisha mnyama kunamuondolewa mawazo."

Pia amesema wakati mnyama amepumzika hatakiwi kupewa chakula cha aina yoyote zaidi ya maji.Ameongeza katika kumchinja mnyama lazima awe amepoteza fahamu kwani naye anaogopa kufa na kwa mazingira hayo mnyama anatakiwa kupigwa shorti ya umeme na kwamba sifa mojawapo ya machinjio ni kuwa na sehemu ya kumpunguzia maumivu.

"Baada ya kuchinjwa damu inadibi iachwe ichuruzike na kuna sababu zake,mojawapo ni kuua balteria na kama inavyofahamika katika damu kuna vitu vingi na ndio maana machinjioni kuna harufu ya damu .Kwa hiyo baada ya mnyama kuchinjwa damu itaachwa itoke na wakati huo huo daftari wanafanya kazi yao ya kuangalia ubora wa nyama.Baada ya nyama kukaguliwa hatua inayofuata ni usafirishaji.Wanatoa huduma hiyo lazima wawe wamepimwa afya, wawe na sare nyeupe,"amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo Jiji la Dodoma Mwesiga Gration amesisitiza umuhimu wa wafanyabiashara ya nyama kuhakikisha mabucha yao yanakuwa salama ili kuwa na nyama iliyobora hasa kwa kuzingatia Jiji la Dodoma wageni ni wengi na lazima wahakikishiwe usalama wa nyama wanayokula na si wageni tu bali na kwa wananchi wote kwa ujumla.

"Leo nipo hapa kuwaomba kwa lugha ya upole kabisa,tuheshimu utaratibu uliopo, nyama iuuzwe katika mazingira safi na salama. Lazima bucha ziwe safi.kuna bucha ukienda unakuta kuna Kigogo kinatumika wakati wa kupata nyama,hii hapana sasa,tubadilike.Dodoma nchi yote iko hapa siko tayari kupoteza kazi kwa ajili ya.kutosimamia yale ambayo natakiwa kusimamia,"amefafanua.

Wakati huo huo Ofisa Usajili Mifugo Bodi ya Nyama Tanzania Geofrey Kakuru amezungumzia usaji wa mifugo na nyama ambapo amesema usajili huo unafanyika kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Bodi ya Nyama Tanzania ambapo wahusika na kusajili maeneo yote yanayohusika na biashara ya mifugo na nyama na hivyo wote ambao wanafanyabiashara hiyo wanatakiwa kusajiliwa na kuna aina nyinyi za wadau ambao wanapaswa kusajiliwa na bodi hiyo.

Ameongeza kwamba sababu za kuwasajili mojawapo ni kuwatambua wadau na wakati huo huo kuwa na nafasi nzuri ya kutatua changamoto zao na kwamba ametoa rai wadau kujisajili. Pia umuhimu mwingine wa kusajili ni kupata takwimu sahihi za masuala yanayohusu sekta ya nyama, kwani hiyo inasaidia hata Serikali inapotaka kufanya jambo lolote katika eneo hilo lazima kuwepo na takwimu sahihi na lengo jingine kusajili kunasaidia katika kuchangia pato la taifa

Hata hivyo amesema kuanzia kesho wataanza kusajili wadau wa nyama na kwamba ni jukumu la kila anayehusika na sekta hiyo kuhakikisha anasajiliwa kwani wasiojisajili watachukuliwa hatua kwani watakuwa wanakiuka sheria
 Wadau wa sekta ya nyama katika Jiji la Dodoma wakiwamo wafanya biashara ya nyama na wamiliki mabucha na wachinjaji nyama wakiwa katika kikao cha kukumbushwa umuhimu wa kufuata sheria katika kutoa huduma ya nyama jijini Dodoma. Kikao hicho kimeandaliwa na Bodi ya Nyama Tanzania ambacho kimefanyika leo   Novemba 28,mwaka 2019
 Ofisa Usajili Mifugo Bodi ya Nyama Tanzania Geofrey Kakuru akifafanua jambo wakati wa kikao cha bodi hiyo na wafanyabiashara ya nyama wakiwamo wamiliki wa mabucha katika Jiji la Dodoma
 Kaimu  Msajili   Bodi ya Nyama Tanznaia Iman Paul Sichwele akizungumza na wafanyabiashara ya nyama na wadau wa sekta hiyo leo Jijini Dodoma
Baadhi ya maofisa kutoka Bodi ya Nyama Tanzania, maofisa Afya na wakuu wa Idara ya Nyama Jiji la Dodoma.wakiwa katika kikao kati yao na wadau wa biashara ya nyama katika Jiji hilo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...