Jeshi la Polisi kanda maalum
Dar es salaam linapenda kutoa tahadhari kwa wakazi wa jiji la Dsm wote kuwa
makini kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepukana na majanga
yanayoweza kuepukika.
Hivyo wananchi wote wanatakiwa kuwa makini na watoto
wadogo wanaohitaji uangalizi wa karibu, pia kujiepusha kupita kwenye maji ya
mito midogomidogo au madimbwi ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wao.
Aidha hadi sasa
zimepokelewa taarifa za watu wawili kufariki dunia kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (SACP) Lazaro Mambosasa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...