Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam linamshikilia Bi Halima Juma (23)Mkazi wa Chalinze kwa tuhuma za
wizi wa fedha kwenye mashine za kutolea fedha (ATM).
Mnamo tarehe 19/11/2019 katika
benki ya CRDB tawi la Mbagala akiwa katika ATM hizo, aidha alimtilia mashaka
binti huyo aliyekuwa kwenye chumba cha ATM ya benki hiyo akijifanya kuwasaidia
wazee na wastaafu wasiojua kutumia ATM mashine vizuri, lakini lengo lake ni
kuchukua namba za siri za wastaafu na wazee hao na kisha kuwabadilishia ATM
kadi zao na baadaye kuwaibia fedha kwenye akaunti zao kwa kutumia kadi halisi
za wahusika baada ya kuwabadilishia kadi na kuchukua namba za siri.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na
askari wanaolinda Benki hiyo na alipopekuliwa alikutwa na ATM kadi 23 za watu
mbalimbali za benki tofauti tofauti zikiwa katika pochi yake huku akiwa
amezificha katika sehemu zake za siri ukeni.
Kadi hizo ni kama ifuatavyo;
1.CRDB kadi 07
2.NMB kadi 06
3.NBC kadi 02
4.AMANA kadi 02
5.POSTA
BENKI kadi 02
6.ACB kadi 01
7.STANIBIC kadi 01
8.DTB kadi 01
9.EQUITY kadi 01.
Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa
na atafikishwa mahakamani hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...