Aliyepo kulia ni Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki,Liberat Mfumukeko akisaini mkataba wa EURO milioni 10 na Balozi wa umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania.Manfredo Fanti (aliyepo kushoto)kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi hizo.



Jumuiya ya Afrika Mashariki imesaini mkataba wa EURO milioni 10 na umoja wa nchi za Ulaya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi uanachama wa jumuiya hiyo.

Mkataba huo umesainiwa mapema leo katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo na Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki ,Liberat Mfumukeko na Balozi wa umoja wa nchi za Ulaya Tanzania ,Manfredo Fanti.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo ,Katibu mkuu wa EAC ,amesema kuwa, fedha hizo zimetolewa na jumuiya ya umoja huo ili kuziwezesha nchi wanachama kukabiliana na changamoto ya usalama ambayo imekuwa na kikwazo kikubwa Cha maendeleo katika nchi hizo.

Ameshukuru jumuiya hiyo kwa msaada huo ambao umekuja muda muafaka na kuongeza kuwa, jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana kwa ukaribu Sana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo ,Mfumukeko amesema kuwa,jumuiya hiyo ya nchi za Ulaya wamekuwa washirikiana kwa muda mrefu na jumuiya hiyo ambapo katika kipindi cha miaka mitano wamekwisha kutoa kiasi Cha EURO milioni 85 .

Kwa upande wake ,Balozi wa jumuiya ya umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Manfredo Fanti amesema kuwa, wataendelea kusaidia jumuiya hiyo katika maswala mbalimbali ya maendeleo .

“tumekuwa tukisaidia jumuiya ya Afrika Mashariki katika miradi mbalimbali tangu mwaka 2007 ambayo imeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo na kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.”amesema Balozi huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...