Na Karama Kenyunko, Michuzi Globu ya jamii

UPANDE wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wako katika mazungumzo na DPP kuhusu kukiri kosa lake lakini bado hawajafika muafaka.

Wakili Jebra Kambole anayemtetea Kabendera, ameeleza hayo leo Novemba 20,mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mapema Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Janeth Mtega kuwa upepelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakili Kambole aliieleza Mahakama kuwa maombi waliyowasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuwa bado wako katika mazungumzo bado hawajafika muafaka, yakikamilika wataitaarifu Mahakama.

Akijibu hoja hiyo Wakili Simon alidai kuwa ni kweli kuna maombi hayo yaliyowasilishwa na upande utetezi ambayo wanayafanyia kazi yatakapokamilika watawataarifu. Hakimu Mtega amahirisha kesi hiyo mpaka Desemba 4, mwaka huu itakapotajwa tena.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.milioni 173.

Inadaiwa katika mashtaka ya kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Pia inadaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh.173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Pia Kabendera inadaiwa alitakatisha Sh.173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...