Na Woinde Shizza Michuzi TV mArusha

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)Mkoa wa Arusha limefanya operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara na wananchi waliojenga makazi ya kudumu katika miundombinu inayosafirisha umeme mkubwa wamsongo wa KV 66.

Umeme huo unaotoka Kituo cha kufua umeme cha Nyumba ya Mungu kuleta mkoani Kilimanjaro hadi mkoani Arusha.Katika operesheni hiyo shirika hilo limevunja zaidi ya maduka 32 na kuwaondoa wamachinga na wafanyabiashara wa vyuma chakavu zaidi ya 20.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha ,Mhandisi Herin Mhina amesema wameamua kufanya hivyo baada ya wananch kukaidi kuondoka kwa hiyari katika maeneo hayo licha
ya uongozi wa shirika hilo kufanya mazungumzo nao na kuwapa
tangazo la notisi miezi miwili.

Amesema walitoa tangazo la kuwataka waliokaa chini ya miundombinu hiyo ya umeme iliopo Kata ya Ungalimited na Daraja mbili ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha Arusha.

"Taarifa zilitolewa toka miezi miwili iliyopita ya kuanza kuwaondoa wafanyabiashara wachache walikubali na walioondoa biashara zao na wengine baadhi walikaidi na kuendelea kufanya biashara zao maeneo hayo na ndio maana wameamua kufanya operesheni ya kuwaondoa.

Amebainisha eneo hilo ni hatarishi maana linapitisha umeme ukubwa ambao ni wa msongo wa kv 66 ambapo laini hiyo iliyojengwa mwaka 1968 na likuwa inatoa umeme kituo cha kufua na kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu kutoka mkoani Kilimanjaro hadi hapa Arusha pamoja

na laini ingine inayopitisha umeme wa msongo wa kv 34.
Amesema kwa mujibu wa sheria za Tanesco wananachi hawatakiwi kufanya biashara yeyote chini ya laini hizo kwani zinaweza kuleta madhara makubwa kwa maisha yao.

"Kama mnavyoona hii laini imevamiwa kwa maana ya watu kuweka shughuli chini ya laini, mkiangalia kwa mbele kunanyumba zimeingia chini ya laini kabisa ,hii laini inatakiwa iwe na korido ya mita 10 kila upande kutokana na ukubwa wake wa msongo wa kv 66.Ndio maana tumeamua kuja kuwatoa na hii sio kwa ajili ya Tanesco tu bali kwa ajili ya usalama wa maisha ya wananchi hawa,"amesema.

Ameongeza kuwa mbali na njia hiyo ya umeme kuna laini zingine mbili
zilizovamiwa ikiwemo ya Monduli ambako kuna watu wameisonga.Laini hiyo ni ya msongo wa Kv 33 na inaitaji korido ya nafasi ya mita tano kila upande ,hivyo ametoa mwito kwa wanachi waliojenga nyumba zao

chini ya miundombinu ya umeme waondoke ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.Amesema wakati wa operesheni hiyo, Mkuu wa kitengo cha usalama sehemu pa kazini Tanesco makao makuu Mhandisi Alexander Budigila amesema operesheni hiyo  halijaanzia katika maeneo hayo pekee bali ni muendelezo wa utekelezai wa sheria ya kutojenga chini ya miundo mbinu ya umeme.

"Sheria hii inatekelezwa nchi nzima, miundo mbinu ya umeme ya TANESCO inatakiwa ilindwe na wananchi wote na sio kuwategemea watumishi wa Tanesco peke yao kwani miundombinu hii ndio inayofanya hata uchumi wa wananchi ukue,"amesema.

Ametoa mwito kwa wananchi wote wazingatie matangazo yanayotolewa na TANESCO kwani ni kwa ajili ya usalama wao na mali zao.Kwa upande wake Ofisa Biashara Jiji la Arusha Godfrey Edward amewataka wafanyabiashara licha ya kufanya biashaa waangalie kwanza sehemu wanazofanyia biashara kama ni salama.

Kuhusu wafanyabiashara ambao mali zao zimechukuliwa wakati wa operesheni hiyo wazifuatilie yadi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha ili walipe faini ya Sh.50000 na kisha kurejeshewa.
 Mafundi kutoka shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha wakiendelea kubomoa vibanda mbalimbali  nantumba vilivyojengwa chini ya njia za umeme mkubwa wa KV 66 unaopita katika kata ya Ungalimited pamoja na
Daraja mbili.(picha na Woinde Shizza,Arusha)
 wafanyakazi wa tanesco wakipakia baadhi ya vitu vilivyokuwa vimewekwa chini ya miundombinu ya umeme mkubwa tayari kanisa kupeleka Katika yadi ya jiji la Arusha

  wafanyakazi wa tanesco mkoa wa Arusha wakipakia kibanda katika gari ya shirika la umeme tayari kabisa kwa kupeleka katika yadi ya halimashauri ya jiji la Arusha ,vitu hivyo vitakaa hapo hadi wamiliki wao wakakomboe 
 Msimamizi wa njia ya kusimamisha umeme kilimanjaro ma Arusha Mhandisi  Pius Josephati akiendelea kuwapimia mita kutoka katika njia za umeme wananchi hao waliojenga kando ya njia hiyo ambapo alibaonisha
kutoka katika nguzo kubwa ya umeme mwamanchi anayakiwa ahache mita kumi(picha na Woinde Shizza,Arusha).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...