Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista
Mhagama, wakati akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma
katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakati alipotembelea mradi wa
nyumba za NHC, zilizopo Mtoni Kijichi katika Wilaya ya Kigamboni, jijini
Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi wa NSSF,
Balozi Alli Siwa, wakati alipokagua Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
wa Taifa na Shirika la Nyumba la Taifa ya Ujenzi wa nyumba Tuangoma,
Mtoni Kijichi na Dungu, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo
Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27,
2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista
Mhagama, wakati akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma
katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwasalimia Watoto wa Chekechea wa Shule ya
Kids Paradise, iliyopo ndani ya Mradi wa Nyumba za NHC, Mtoni Kijichi
wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, wakati alipokagua Miradi ya
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa na Shirika la Nyumba la Taifa ya
Ujenzi wa nyumba Tuangoma, Mtoni Kijichi na Dungu, Novemba 27, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za Watumishi Housing,
uliyopo Dege wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27,
2019.



****************************************
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema nyumba zote zinazojengwa na Taasisi za
Umma katika wilaya Kigamboni jijini Dar es salaam zinapaswa kukamilika
haraka ili ziuzwe ua kupangishwa kama ilivyokusudiwa.
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Novemba 27, 2019) baada ya kukagua miradi ya ujenzi
wa nyumba za NSSF, NHC na Watumishi Housing iliyopo katika wilaya ya
Kigamboni.
Waziri
Mkuu amesema inasikitisha kuona kwamba watumishi wa umma na wananchi
jijini Dar es Salaam hawana nyumba nzuri za kuishi wakati zipo nyumba
nyingi nzuri zimejengwa na zinahitahi umaliziaji mdogo tu ili ziweze
kukalika.
Hivyo,
Waziri Mkuu ameitaka Menejimenti ya NSSF kakamilisha haraka ujenzi na
uwekaji wa miundombinu ya umeme, maji safi na maji taka katika nyumba
zake 161 zilizoko Tuangoma, 820 zilizoko Mtoni Kijichi na 439 zilizoko
Dungu ili ziuzwe na kuepusha uwezekano wa uharibifu unaoweza kutokea kwa
nyumba hizo kakaa muda mrefu bila kupata wanunuzi au wapangaji.
Ili
kufanikisha jambo hilo Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mthamini Mkuu wa
Serikali atathimini nyumba hizo na kutoa bei halisi ya soko kwa sasa ili
kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na
kupanga katika nyumba hizo.
Pia,
Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa wilaya na viongozi wa Halmashauri ya
wilaya ya Kigamboni kuwasaidia watumishi wa wilaya na Halmashauri hiyo
kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi hao kupewa kipaumbele
katika kununua au kupanga kwenye nyumba hizo.
Mheshimiwa
Majaliwa pia ameitaka Menejimenti ya NSSF kufikiria namna ya kuzungumza
na viongozi wa vyuo mabalimbali kama vile Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM), Chuo cha Mwalimu Nyerere ili wanafunzi wa vyuo hivyo wapatiwe
fursa ya kupanga katika nyumba hizo kwa bei watakazomudu.
Pia
Mheshimiwa Majaliwa ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam
ukishirikiana na SUMATRA kuanzisha njia za mabasi ya daladala
zitakazoanzia au kupitia kwenye nyumba za NSSF Mtoni Kijichi na Dungu
ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua nyumba hizo kupata
usafiri wa umma.
Vilevile,
Waziri Mkuu ameuagiaza uongozi huo kuhakikisha kwamba eneo la Mtoni
Kijichi zilipojengwa nyumba za NSSF na NHC linapata huduma za Shule,
Kituo cha Afya na Kituo cha Polisi kwani litakuwa na wakazi wengi .
Ili
kuongeza thamani ya nyumba hizo na kuvutia wapangaji na wanunuzi,
Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Menejimenti ya NSSF kuboresha barabara
kwenye mitaa yote zilipojengwa nyumba hizo kwa kushirikiana na TARURA.
“Nashauri
ziwekwe taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya nyumba hizi ili
kupendezesha eneo na kuwafanya wananchi wahamasike kununua na kuishi
katika nyumba hizi” amesema Majaliwa.
Akiwa
kwenye Mradi wa Nyumba za NHC Mtoni Kijichi, Mheshimiwa Majaliwa
alitembelea Shule ya Awali ya Kids Paradise na kufurahishwa na utaratibu
mzuri wa shirika hilo wa kukumbuka kujenga jengo zuri la Shule hiyo na
kulipangisha ili kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi katika nyumba hizo
wanapata fursa ya kusoma elimu ya awali.
Akizungumza
baada ya kukagua Mradi wa ujenzi wa nyumba za NHC Mwongozo, Mheshimiwa
Majaliwa ameutaka uongozi wa NHC kuwa karibu na wateja wanaopanga au
kununua nyumba zao. “ Shughulikieni malalamiko yote yanayotolewa na
wateja wenu ili wajenge imani kwenu, Alisisitiza Majaliwa.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu Jenista Mhagama alisema wizara yake imeyapokea maelekezo yote
yaliyotolewa na Waziri Mkuu na kwamba watafanya kila njia ili
kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au
kupangishwa.
Naye
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, william Lukuvi
alimwambia Waziri Mkuu kuwa amekwishatoa maagizo kwa NHC ijenge uzio
japo wa waya na wapande michongoma ili kuweka ulizi kwenye eneo la
nyumba zao za Dungu.
Mheshimiwa
Lukuvi alisema amewapa NHC miezi mitatu ili wafanye marekebisho katika
nyumba ambazo zimelalamikiwa na wateja kuwa zina kasoro ili kujenga
imani kwa wateja wao.
Mapemba
Mkadiriaji Majengo wa NSSF, Abon Mhando ambaye pia ni Kaimu Meneja wa
Miradi wa NSSF alimwambia Waziri Mkuu kuwa Mradi wa ujenzi wa nyumba wa
Tuangoma una jumla ya nyumba 161 na kati ya hizo nyumba 76 zimekamilika.
Aliwataja wakandarasi wanaojenga mradi huo kuwa ni Kampuni za CASCO,
Advent na NANDRA.
Alisema
Mradi wa Dungu una jumla ya nyumba 439 na kati ya hizo nyumba 95
zimekamilika na jumla ya makampuni 13 yameshiriki katika ujenzi wa mrdi
huo.
Kuhsu mradi wa Mtooni Kijichi Mhando alisema mradi huo una jumla ya nyumba 820 na kati ya hizo nyumba 417 zimekamilika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...