Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI),
Mh. Suleiman Jaffo (kulia), Mkurugenzi wa M-Pesa (katikati) Epimack
Mbeteni pamoja na Mkurugenzi wa Vodacom Business, Arjun Dhillon
(kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa
Ushirikiano baina ya
TAMISEMI na Vodacom ambao utawezesha Ofisi 127 za serikali za mitaa kupokea malipo kupitia M-Pesa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Mh. Suleiman Jaffo (kulia), Mkurugenzi wa M-Pesa Epimack Mbeteni (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Vodacom Business, Arjun Dhillon (kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Ushirikiano baina ya
TAMISEMI na Vodacom ambapo zaidi ya wateja milioni 14 watanufaika na matumizi ya M-Pesa katika malipo ya halmashauri na manispaa kote nchini.
************************************
· Zaidi ya wateja milioni 14 kunufaika na matumizi ya M-Pesa katika malipo ya halmashauri na manispaa kote nchini.
Novemba 3, 2019. Dar es Salaam: Wateja zaidi ya milioni 14 wa Vodacom watanufaika na huduma ya malipo kwa M-Pesa kwenda halmashauri na manispaa mbali mbali nchini. Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na ofisi ya TAMISEMI wamefanikisha kuimarisha mfumo wa malipo ya kifedha kwa kusogeza huduma ya malipo kwa M-Pesa kwa ofisi zaidi ya 127 za serikali za mitaa nchini. Uzinduzi wa huduma hiyo, ulifanyika ofisi za Makao Makuu ya Vodacom, Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa. Suleiman Jaffo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mh Jaffo alisitiza umuhimu wa kutumia njia za kidigitali kama M-pesa kufanya malipo na kukusanya mapato kwani itaboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza uvujaji na ubadhirifu wa pesa za umma pamoja na kuongeza mapato kwa idara mbalimbali za Serikali za mitaa.
“Malipo kutumia njia hizi za kidijitali yanapunguza muda mwingi tuliokuwa tunatumia kupanga foleni kufanya malipo. Sasa tuna M-Pesa naamini muda huu tutaupeleka moja kwa moja kwenye kujenga taifa na shughuli za maendeleo. Napenda kuwapongeza Vodacom kwa kutukumbuka na sisi huku TAMISEMI. Ninatumaini kwamba huduma hii itawarahisishia malipo, si tu kwa wananchi bali hata nyinyi viongozi katika kutunza hesabu zenu, usalama wa fedha pamoja na ukusanyaji fedha kwa ujumla,” aliongeza Jaffo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa huduma ya M-Pesa, Bwana Epimack Mbeteni alisema kupitia M-Pesa, Vodacom inategemea kufikia taasisi nyingi za serikali na binafsi ili kuwezesha mfumo wa malipo kuwa rahisi, fanisi na salama zaidi.
“Asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia M-Pesa kufanya miamala mbalimbali kama Luku, bili za maji, faini za barabarani, ndio maana tukaona fursa kubwa ya kurahisisha malipo kwa serikali za mitaa kutumia M-Pesa,” aliongeza Mbeteni.
Ushirikiano huu baina ya TAMISEMI na M-Pesa utawawezesha wateja wa mtandao wa Vodacom kufanya zaidi ya malipo 205 ya serikali za mitaa kwa urahisi na usalama zaidi. Malipo kama vile leseni za biashara, vibali vya ujenzi, malipo ya maegesho na nyinginezo.
“Wote tunashuhudia jinsi M-Pesa inavyoendelea kubadilisha mfumo wa malipo nchini, ni tegemeo letu kwamba, malipo katika serikali za mitaa yatakuwa rahisi na salama zadi,” alisema Mbeteni.
Ili kulipa kupitia M-Pesa unapiga *150*00# halafu chagua lipa kwa M-Pesa, halafu malipo kwa serikali kisha weka namba ya kumbukumbu ambayo utapewa na ofisi za serikali za mtaa au unaweza kutumia APP ya M-Pesa kufanya malipo wakati wowote,” alifafanua Mbeteni.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...