Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

JUMLA ya wakimbizi 330,765 kutoka Rwanda, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) na wengine kutoka nchi 15 wamepata hifadhi nchini pamoja na kupata huduma muhimu ikiwemo elimu na afya.

Akizungumza leo Novemba 28,2019 jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya takwimu duniani Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema mwaka 2018 Serikali kwa kushirikiana na Shirika linaloshughulikia wakimbizi (NHCR) lilianzisha mfumo rasmi kwa utoaji kwa elimu ya msingi ambapo asilimia 90 ya watoto kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na asilimia 79 ya watoto kutoka Burundi waliandikishwa kupata elimu ya msingi.

Mpango amesema Tanzania itaendelea kuwagharamia wakimbizi na wale wenye uhitaji wa hifadhi na kueleza kuwa hadi sasa jumla ya wakimbizi laki mbili wakiwemo wake, waume na watoto wamepewa uraia wa Tanzania.

Aidha amewataka watakwimu wote katika Halmashauri zote nchini kuripoti kwa Mtakwimu mkuu wa Serikali na hiyo ni  kutokana na uwepo wa wakimbizi wengi katika halmashauri nyingi hivyo hitaji kupata takwimu ni kubwa hasa kwa kujua na kutambua mahitaji yao ya muhimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa Albina Chuwa amesema  maadhimisho hayo ya siku ya takwimu hufanyika kila mwaka  Novemba 28, na kwa mwaka huu maadhimisho hayo yataende sambamba na kujadili changamoto zinazozikumba Chama cha takwimu nchini na  tasnia hiyo kwa ujumla.

Amesema, wamekuwa wakikusanya takwimu mbalimbali kupitia sensa za watu na makazi na baadaye kupima na kutoa takwimu sahihi kulingana na mahitaji muhimu.

"Siku ya takwimu inayoadhimisha kila mwaka imewalenga wananchi, wapate kujifunza kuhusiana na takwimu na leo  tutajadili changomoto mbalimbali na wadau wakiwemo wananchama wa chama cha takwimu duniani lakini pia tutajadili namna ya kuboresha tasnia hii" ameeleza.

Ameeleza kuwa wananchi wanahitaji kupata takwimu sahihi na Ofisi hiyo itaendelea kutoa elimu ya takwimu kupitia majukwaa mbalimbali kwa manufaa ya jamii kwa ujumla. 
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Jamvi la Habari Veronika Mrema,akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango ,Veronika amekuwa mshindi wa pili katika tuzo za Waandishi wa Kitakwimu zilizotolewa leo Novemba  28,2019 na Ofisi ya Takwimu ya Taifa.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa Siku ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri ametoa maagizo kwa Ofisi ya Takwimu (NBS), na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  kufanya kazi kwa kushirikiana. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Amina Msangi Akizungumza katika Mkutano wa Siku ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo kauli mbiu ilikuwa ni ‘Kila mmoja wetu ana umuhimu kwa takwimu bora, kwa usimamizi bora wa watu wanaolazimika kuyakimbia makazi yao barani Afrika’
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa akizungumza katika na Washiriki wa Mkutano wa Siku ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo kauli mbiu ilikuwa ni ‘Kila mmoja wetu ana umuhimu kwa takwimu bora, kwa usimamizi bora wa watu wanaolazimika kuyakimbia makazi yao barani Afrika’ 
  Mkurugenzi Msaidizi-Idara ya Ajira na Ukuzaji Ajira, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Ahmed Makbel akichangia mada katika Mkutano wa Siku ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo kauli mbiu ilikuwa ni ‘Kila mmoja wetu ana umuhimu kwa takwimu bora, kwa usimamizi bora wa watu wanaolazimika kuyakimbia makazi yao barani Afrika’. 
 Sehemu ya meza kuu akifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo 

 Sehemu ya Wadau wa Watakwimu kutoka Sehemu mbalimbali nchini wakifuatilia Mkutano wa Siku ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Novemba 28, 2019, kauli mbiu ilikuwa ni ya Mkutano huo ni ‘Kila mmoja wetu ana umuhimu kwa takwimu bora, kwa usimamizi bora wa watu wanaolazimika kuyakimbia makazi yao barani Afrika’
 
Wanafunzi kutoka Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika waliohudhuria katika Siku ya Takwimu Afrika iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakifuatilia Mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...