*Ni baada ya video kusambaa mtandaoni akionesha mtu akitishwa kwa bastola
*Waziri asema hata kiwembe nacho ni silaha,marufuku kumtisha nacho mtu
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii
BAADA
ya kuwepo picha ya video mtandaoni inayoonesha kuna mtu ameshika silaha
aina ya bastola akimtisha mtu mwingine, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi
Lugola amesema ni kosa kisheria kwa anayemiliki silaha kutaka kuitumia
kinyume na sheria na atakayekamatwa atachukuliwa hatua kwani hakuna
aliyekuwa juu ya sheria.
Akizungumza
leo Novemba 2,2019 jijini Dar es Salaam ,Waziri Lugola amesema ni kosa
kisheria kutumia silaha kumtisha mtu au kutaka kumdhuru nayo ." Kwetu
sisi wembe,kisu,upinde na aina nyingine ya silaha ni marufuku kumtisha
nayo mtu.
"Ipo sheria ya
kumiliki silaha, kuitumia na namna ya kuihifadhi.Hivyo kwa wanaomiliki silaha za moto lazima waheshimu sheria ,ni vema Watanzania wote wakawa
makini na matumizi ya silaha,'amesema Waziri Lugola.
Hata
hivyo amesema kuna mkakati unaandaliwa kupitia Kampuni ya Jeshi la
Polisi watatoa mafunzo kwa watu wote wanaomiliki silaha za moto ili
kuhakikisha wanazitumia kwa matumizi sahihi na mafunzo hayo yanaweza
kutolewa kwa gharama ndogo ya fedha.
"Kila
anayemiliki silaha lazima apewe mafunzo ya matumizi bora ya silaha.
Hiyo itasaidia kuwakumbusha silaha inahifadhiwa vipi na inatumika
vipi.Hata sisi Polisi tumekuwa na utaratibu wa kwenda mafunzo ya mara
kwa mara.
"Ambapo huko
pia tunakumbushana kuhusu matumizi ya silaha,hivyo lazima na raia ambao
wanamiliki silaha wapate mafunzo,"amesema na kuongeza mafunzo hayo
yatahusu na ulengaji shabaha.
Hata hivyo amesema
sheria ya kumiliki silaha ya moto iko wazi,hivyo yoyote ambaye atakiuka
atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,"amesema Waziri Lugola.
Wakati
huo huo amesema katika ziara yake ya kikazi ambayo ameifanya katika
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ameona kazi zinavyofanyika kwa
weledi,umakini na ujuzi huku akisifu namna askari Polisi
wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku na kwamba wanastahili pongezi.
Akiwa
katika ziara hiyo amepata nafasi ya kuona kazi zinazofanywa na jeshi
hilo katika Kitengo cha kuzuia uhalifu mtandaoni ambapo amesema kuna
mambo ambayo wamekubaliana ili kufanikisha utendaji kazi.Hata hivyo
amesema Polisi wamefanikiwa Kudhibiti matukio ya uhalifu yakiwemo ya
wizi mtandaoni .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...