Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson

Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii

CHAMA cha Conservative kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kimeshinda kwa kishindo baada ya kujinyakulia viti zaidi ya 300 katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika jana  Desemba 12.

 Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya matokeo hayo kutangazwa na chama chake kushinda viti 364 na na kuvuka idadi ya viti 326 walivyotakiwa kupata ili watangazwe kuwa washindi, Boris ameviambia vyombo vya habari kuwa Serikali hiyo mpya ni hatua muhimu katika kutekeleza demokrasia kwa raia na kujenga uimara wa kuimarisha taifa hilo.

Kutokana na ushindi huo mnono Boris amesema kuwa hiyo ni nafasi adhimu na nafasi ya kufanikisha Brexit na kuiondoa Uingereza katika Muungano wa nchi za Ulaya.

Amewashukuru wananchi waliojitokeza siku ya jana kuanzia saa moja asubuhi hadi saa nne usiku katika kupiga kura ambazo zimeleta mapinduzi katika makubwa katika taifa hilo na amehaidi kuwa Serikali hiyo itaheshimu maamuzi na demokrasia katika taifa hilo na wananchi wake.

Kwa niaba ya wateule hao Boris amehaidi kufanya kazi kwa bidii zote kama wananchi hao walivyoonesha uaminifu katika zoezi la kupiga kura na kupelekea ushindi wa chama hicho ambacho kimenyakua baadhi ya viti kutoka chama pinzani cha Labour ambapo kiongozi wa chama hicho Jeremy Corby amesalimu amri na kueleza kuwa hataongoza chama hicho mwakani.

Chama pinzani cha Labour  kimepoteza nafasi katika majimbo ya Wales na Kaskazini mwa England maeneo ambayo yalipiga kura za kutosha za nchi hiyo kujiondoa katika umoja wa Ulaya (Brexit) mwaka 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...