Akizungumza na wadau waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
Dkt.Amos Nungu amesema, lengo ni kutafiti, na kutoa elimu pamoja na kuendeleza
sekta baianuai(biodiversity) inahusisha mgawanyiko wa maisha ya wanyama na
mazingira.
Amesema lazima jitihada za makusudi zichukuliwe ili data
ziweze kuhifadhiwa na tafiti ziweze kufanywa ambazo zitaelimisha sisi tuliopo
na vizazi vijavyo.
"Kwahiyo tunamradi wa pamoja kati ya DIT na COSTECH,
lakini sisi ni watekelezaji tuu, wadau wa mradi huo ni taasisi mbalimbali
kulingana na majukumu yetu, tunaongelea mazingira na utalii nchini, sasa kusudi jitihada zichukuliwe ili kuhifadhi,
kutunza, na kufanya tafiti ambazo zinaelimisha, sisi tuliopo na vizazi
vijavyo".
Dkt.Nungu amesema kuwa watafiti washirikiane pamoja katika
kuibua data na taarifa kwaajili ya kuendeleza na kuhifadhi kwa maendeleo ya
nchi.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaam Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Utawala na Fedha, Najat
Mohamed amesema, mradi huu ni mhimu kwa taifa letu, ambao utatengeneza mfumo
wa kieletroniki wa kuhifadhi kumbukumbu
za baianuai(biodiversity), kwa kuwezesha kuapata taarifa za viumbe hai
mbalimbali.
"Mradi wa kutengeneza mfumo wa kuhifadhi na kusambaza
taarifa za baianuai(biodiversity) hapa nchini na kuwezesha upatikanaji wa taarifa hizi kwa wadau na kwa matumizi mbalimbali
".
Amesema taarifa za baianuai(biodiversity) ni mhimu kwa
mipango ya kiuchumi na uhifadhi wa mazingira yetu.
"Taarifa za baianuai(biodiversity) ni mhimu kwa
maendeleo ya taifa lolote, maana bila
viumbe hai hakuna maisha, bila mimea, wanyama na wadudu maisha ya binadamu
yatakuwa hatalini maana ndio vyanzo vya
chakula, hali ya hewa nzuri, mvua na mahitaji mengine ya binadamu kama
dawa".
Amesema kuwa tume ya Sayansi na Teknolojia kupitia wataalamu
wake iliandaa andiko la mradi likiwa na
lengo la kufanya utafiti na kutengeneza mfumo wa kieletroniki wa kuhifadhi na
kutoa taarifa za baianuai(biodiversity) ya Tanzania kwa wadau mbalimbali.
Hata hivyo Mwenyekiti wa taarifa za, baianuai(biodiversity)
Tanzania, Profesa Pantaleo Munishi amesema baianuai(biodiversity)ni msingi wa
maisha hapa duniani kwani kila kiumbe hai kinachoonekana ni
baianuai(biodiversity).
"Baianuai(biodiversity) ni chanzo cha mahitaji mengi
sana ya binadamu, mazao ya kilimo, mazao ya misitu, mazo ya majini, na vyakula
aina mbalimbali pia ni chanzo cha uchumi".
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa kusaini makubaliano ya kutunza data na taarifa mbalimali za mazingira na wanyama.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Utawala na Fedha, Najat Mohamed akizungumza wakati wa kusaini makubaliano kati ya DIT na tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu.
Baadhi ya viongozi wa DIT na COSTECH waliofika kushuhudia utiaji saini katika mikataba hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu na Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Utawala na Fedha, Najat Mohamed wakisaini mkataa leo jijini Dar es Salaam, kwaajili ya kutengeneza mfumo wa kielektroniki amao utahifadhi data za bainowai.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu na Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Utawala na Fedha, Najat Mohamed wakibadilishana mikataa jijini dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...