Kamanda wa Kikosi cha Polisi Tazara, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Advera Bulimba akizungumza na abiria wanaosubiri kusafiri na treni kutokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya na Zambia. Kamanda Bulimba ametoa onyo kwa wahalifu wanaohujummu miundombinu ya reli kuacha mara moja na amewaomba wananchi wanaoishi jirani na reli kutoa taarifa wanapoona uhalifu wa kuiba mataruma ya reli unatendeka.

KATIKA KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA, KAMANDA WA KIKOSI CHA POLISI TAZARA (DPC) KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI, ACP ADVERA BULIMBA AMEWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU WANAOWAIBIA ABIRIA WANAOSAFIRI NA TRENI ZA RELI YA TAZARA NA WALE WANAOHUJUMU RELI HIYO KWA KUNG’OA MATARUMA YA RELI.
KAMANDA BULIMBA AMESEMA KIKOSI CHAKE KIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA WANALINDA MIUNDOMBINU YA RELI NA KUHAKIKISHA USALAMA WA ABIRIA WANAOSAFIRI KUPITIA RELI HIYO WANAKUA SALAMA WAKATI WOTE WA SAFARI YAO.
AMEONGEZA KUWA, WAPO BAADHI YA WATU WASIO WAAMINIFU AMBAO HUPENDA KUTUMIA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI KWA KUWAIBIA ABIRIA AMA KUHUJUMU NJIA YA RELI.
AIDHA , KAMANDA BULIMBA AMESEMA KUWA KIKOSI KIMEJIPANGA VIZURI NA TAYARI ASKARI WA INTELIJENSIA, MAKACHERO NA ASKARI WA MBWA WAMESAMBAZWA MAENEO MBALIMBALI YA KIKOSI HICHO KUANZIA TAZARA DAR ES SALAAM HADI TUNDUMA.
AMETOA ONYO KALI WENYE TABIA ZA KIHALIFU KUACHA MARA MOJA NA ATAKAETHUBUTU KUFANYA UHALIFU WOWOTE WATAMCHUKULIA HATUA KALI ZA KISHERIA.
ALIONGEZA KUWA TAZARA NI MOJA YA CHANZO CHA KUINGIZA MAPATO YA NCHI, NA ILI KUFIKIA MAFANIKIO HAYO, NI LAZIMA USALAMA WA MALI NA WATU WANAOTUMIA RELI YA TAZARA UIMARISHWE NA NDI MAANA KIKOSI HICHI KIPO NA KIPO IMARA NA WATAHAKIKISHA MAPATO YANAYOTOKANA NA RELI YA TAZARA HAYATA HUJUMIWA NA MTU YEYOTE.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...