Na Khadija Seif, Michuzi TV

MCHUMBA wa Msanii wa kike wa Bongomovie  Elizabeth Michael maarufu Kama Lulu, Francis Siza almaarufu Dj Majizzo ameonesha kumkubali Mrembo huyo kwa uvumilivu wake kipindi chote tangu amvishe Pete mwanzo mwa mwaka huu na kuhudhuriwa na watu lukuki akiwemo rafiki yake wa karibu Dk. Cheni.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa Majizzo ameandika ujumbe kama ishara ya kuonyesha kumkubali Lulu.

"Nakukubali mshikaji wangu japo mwaka umeisha na ndoa haina dalili lakini bado hujanikatia tamaa nakukubali Sana,"

Aidha, Mrembo huyo wa tasnia ya Bongomovie hakusita kumjibu mchumba wake .

"Nakukubali bro, Mswahili Numero uno tushakuwa ndugu tena maana umenipiga password mpaka tumeanza kufanana yote kheri 2019 nimekosa wedding nimepata twin,"

Hata hivyo Majizzo amempongeza mwanadada Maua sama kwa kuingia jukwaani kwa aina yake akiwa juu ya chuma na kulitendea haki jukwaa la tamasha Muziki mnene lililofanyika wiki iliyopita katika viwanja vya Tanganyika Packers kawe jijini Dar es salaam.

"Waswahili tulikua na hofu kama umeweza kupanda kwenye stage ukiwa juu ya hilo chuma,haikuwa ngumu kwako ukatimiza majukumu yako.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...