Mkuu wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS), Bi. Rehema Mligo akielezea namna ambavyo wanafunzi wa uuguzi wanaosoma katika Taasisi hiyo wanavyopatiwa mafunzo ya vitendo katika maabara ya kisasa ya ujuzi iliyopo katika taasisi hiyo mbele ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya), Bw. Gerald Chami(kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu huduma ya Maktaba inayotolewa na Taasisi hiyo toka kwa Mkuu wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS), Bi. Rehema Mligo (katikati) wakati wa ziara ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jijini Dodoma. Kulia ni Mkutubi wa Maktaba hiyo, Andrew Gerald. Ziara hiyo ni muendelezo wa Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake kuelezea maboresho yanayofanywa katika sekta ya Afya chini ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...