Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko
akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa
Maafa nchini leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019.kulia kwake ni
Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja, Selestine Masalamando.

Mkurugenzi Idara
ya Uratibu wa Maafa , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy
Matamwe,akieleza umuhimu wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini
wakati wa kikao cha Jukwaa hilo, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba,
2019.kulia kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko na Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha
Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja,
Selestine Masalamando.

Baadhi ya wajumbe
wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakifuatilia kikao cha
Jukwaa hilo leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019. Jukwaa hilo
hutathmini na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa serikali kuhusu majanga ya
aina zote.

Mratibu wa
masuala ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Charles Msangi akifafanua
umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau katika usimamizi wa maafa wakati wa
kikao cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini leo jijini
Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019

Wajumbe wa Jukwaa
la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakiwa katika kikao cha Jukwaa
hilo, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019, Jukwaa hilo linaundwa
kwa kuzingatia kifungu cha 40 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya
mwaka 2015.

Wajumbe wa Jukwaa
la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi.
Dorothy Mwaluko leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019, Jukwaa hilo
linaundwa kwa kuzingatia kifungu cha 40 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa
Na. 7 ya mwaka 2015.

Baadhi ya wajumbe
wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakifuatilia kikao cha
Jukwaa hilo leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019, Jukwaa hilo
linalojukumu la kufuatilia utekelezaji wa Mkakati wa Kupunguza Madhara
ya maafa wa Sendai, 2015-2030.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
*******************************
Na. OWM DODOMA
Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko
amelielekeza Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini kutoa ushauri
wa kitaalamu unaojikita katika hatua ya kabla ya maafa kutokea na sio
kujikita wakati wa maafa yanapotea kama ilivyozoeleka, kwa kuwa ushauri
wa namna ya kuzuia na kujiandaa na maafa kabla ya maafa kutokea huweza
kupunguza madhara ya maafa na rasilimali zinazohitajika katika
upunguzaji wa madhara hayo.
Ameyasema hayo
leo Jijini Dodoma, wakati akifungua kikao cha Jukwaa hilo ambapo
amebainisha kuwa wakati wa kukabili majanga na maafa kunakuwepo na
mipango mingi ambayo hutekelezwa na wadau wa menejimenti ya maafa na kwa
uchache wakati wa urejeshaji hali wa maafa, lakini mipango ya
kujiandaa na kuzuia maafa ambayo hufanyika kabla ya maafa kutokea kwa
ajili ya kuzuia au kupunguza madhara ya maafa yatakapotokea huwa
haitekelezwi.
“Tumekuwa na
maafa hapa nchini ambayo yameleta madhara nchini, itakumbukwa ajali ya
moto mjini Morogoro hivi karibuni, tujiulize kuna mipango inayoendelea
katika kuzuia majanga hayo, yapo maafa ya mvua yanaendelea kutokea,
lakini je ipo mipango ya kabla ya maafa kutokea, lakini pindi maafa
yakitokea wadau wa menejimenti ya maafa hujitokeza na kuanza kukabili
maafa, sasa nataka nguvu nyingi ielekezeni kwenye mipango ya kabla ya
maafa kutokea na hata ikibidi ainisheni majanga yanayoweza kutokea
kwenye maeneo husika ili jamii iweze kujiandaa na kuyazuia maafa husika
kabla yakutokea“ Amesisitiza Mwaluko.
Aidha,
amelielekeza Jukwaa hilo kuupitia Mkakati wa Taifa wa Kupunguza athari
za maafa na kuhakikisha kuwa unaendana na uhalisia wa hali ya majanga
yanayotokea katika jamii ili uweze kutekelezeka kwa kuweka malengo yenye
uhalisia, huku akisisitiza kuwa ni vyema mkakati huo ukatafsiriwa kwa
Kiswahili ili uweze kutumiwa vyema na walengwa kuanzia ngazi ya msingi
ya maafa ambayo ni kamati za vijiji.
Katika hatua
nyingine Bi. Mwaluko amelielekeza Jukwaa hilo kuwa na ushirikiano
miongoni mwa wadau wa jukwaa hilo kwa kila mdau kuainisha majukumu yake
na namna anavyoyatekeleza majukumu yake, ili kuweza kujua jukumu la kila
mdau na anafanya nini na kwa wakati gani na hatimaye mipango ya
kuimarisha Usimamizi wa maafa iwe inayotekelezeka.
“Kupunguza
madhara ya maafa ni suala mtambuka lenye mchango mkubwa katika shughuli
za maendeleo.Wakati mwingine wananchi wamekuwa wakipata madhara kwa
kukosa uelewa hivyo ni vyema kila mdau kuwajibika katika majukumu yake
kwa kutoa fursa ya uratibu wa usimamizi wa maafa kwa ushirikiano wa
wataalamu wa fani mbalimbali” Amesema , Bi. Mwaluko.
Awali akiongea
katika kikao hicho, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa , Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, ameeleza kuwa Jukwaa hilo ni chombo
cha kisheria ambacho lipo kwa ajili ya kutathmini na kutoa ushauri wa
kitaalam kwa serikali kuhusu majanga ya aina zote, ambapo Jukwa hilo
linaundwa kwa kuzingatia Kifungu cha 40 cha Sheria ya Usimamizi wa
Maafa Na.7 ya mwaka 2015.
Jukwaa hilo
ambalo linajumuisha wataalamu wa fani mbali mbalimbali kwa kujumuisha
sekta ya umma na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na umoja wa
mataifa na asasi za kiraia jukumu lake la msingi ni kutoa ushauri
maeneo ya kipaumbele katika usimamizi wa maafa kwa uratibu na
ushirikishawaji wa wadau ili kufanikisha kujumuisha upunguzaji wa
madhara ya maafa katika mipango na sera za maendeleo ya taifa na katika
misaada ya kibinadamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...