Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imepanga kuongeza uzalishaji mara mbili wa zao la mpunga kutokea tani Milioni 2.2 hadi kufikia tani Milioni 4.5 ifikapo mwaka 2030 lengo likiwa ni kutokomeza kabisa tatizo la njaa nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga leo jijini Dodoma alipokua akizindua mkakati wa Taifa wa miaka 10 wa kuongeza uzalishaji wa kilimo cha mpunga na kuwajengea uwezo wakulima wa kufanya kilimo chenye tija zaidi kibiashara.
Mhe Hasunga amesema hilo litafanikiwa kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, kuzingatia matumizi ya mbegu bora, mbolea, dawa zinazofaa, zana bora za kilimo na kupunguza upotevu kabla na baada ya mavuno.
Amesema amefurahishwa na matokeo yanayoonesha Tanzania imeshika nafasi ya nne kwa uzalishaji wa zao la mpunga lakini akasikitishwa kuona tunazidiwa na Nchi kama Madagascar ambayo haina ardhi yenye rutuba na bora kama yetu.
" Nafasi ya nne siyo mbaya lakini sisi ni Nchi iliyobarikiwa zaidi kulinganisha na Misri, Madagascar ambao wametupita. Nitafarijika zaidi tukipanda hadi nafasi ya pili," Amesema Waziri Hasunga.
Ameielekeza Wizara yake kuongeza uzalishaji wa mbegu bora, kuongeza eneo toka milioni 1.1 hadi 2.2 ifikapo 2030 na kuongeza thamani ya zao la mpunga.
Amesema kuna kila sababu ya kusonga mbele katika zao hilo hasa ukizingatia zao ni pendwa na kila mtu na wanaweza kutoa mchele safi na bora ambao unaweza kuuzwa katika nchi mbalimbali na kutaka mkakati huo unaoanza 2019 -2030 ukawe chachu ya maendeleo ya wakulima wa zao hilo hapa nchini.
Nae Katibu Mkuu wa wizara hiyo mhandisi Methew Mtigumwe amesema Tanzania imedhamiria kuongeza uzalishaji wa zao hilo la mpunga kwa kuongeza hekta kutoka milioni 1.1 hadi kufikia hekta milioni 2.2 mwaka 2030.
" Mkakati huu tuliozindua leo ni muendelezo wa matokeo ya utekelezaji wa mkakati wa awali wa kuendeleza zao la mpunga NDRS 1 ambapo ili kuongeza kiwango cha uzalishaji uliowekwa ni lazima kupanua maeneo yanayofaa kwa kilimo cha mpunga kwa umwagiliaji na yale yanayotegemea mvua," Amesema Mhandisi Mtigumwe.
Amewashukuru Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kwa kuwa nao pamoja katika mchakato mzima wa maandalizi ya mkakati huo.

Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga akizindua mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la Mpunga kufikia tani 4.5. Mkakati huo ni wa miaka 10 kuanzia 2019/20 hadi 2029/30.
Waziri
wa Kilimo, Mh Japhet Hasunga akizungumza na wadau wa kilimo ambao
wamejitokeza katika uzinduzi wa mkakati maalumu wa kuongeza uzalishaji
wa zao la kilimo nchini kufikia tani 4.5 ifikapo mwaka 2030
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...